Thursday, December 2, 2010

Urusi yadaiwa kuongozwa na Genge la Mafia - Wikileaks



Taarifa za hivi karibuni zilizochapishwa na mtandao wa Wikileaks, zinamnukuu mwendesha mashataka mmoja kutoka Uhispania akisema kuwa serikali ya Urusi inaendeshwa na genge la mafia.

Jaji Jose "Pepe" Grinda Gonzales alielezea ubalozi wa Marekani mjini Madrid kuwa hali hiyo pia inashuhudiwa nchini Belarus and Chechnya.

Mawasiliano hayo yaliochapishwa na gazeti la The Guardian yanamnukuu akisema kuwa ni vigumu kutofautisha mikakati ya serikali katika nchi hizo na ile ya magenge hayo ya mafia.

Jaji Gonzales ambaye pia aliongoza uchunguzi kuhusu harakati za kundi la mafia kutoka Urusi nchi mwake, pia anahoji ikiwa Waziri Mkuu Vladimir Putin anashirikiana na kundi hilo.

Mtandao wa Wikileaks umekuwa ukifichua maelfu ya nyaraka za siri za mawasiliano kati ya mabalozi wa Marekani kuhusu viongozi wa nchi wanazowakilisha.

Serikali ya Marekani imeomba radhi kufuatia ufichuzi huo.

Rais Barack Obama amemteua Russell Travers, mtalaamu wa masuala ya Ugaidi kuchunguza jinsi Wikileaks ilivyopata nyaraka hizo na kuimarisha usalama kwenye mtandao wa mawasiliano ya serikali. (BBC Swahili)

No comments: