Saturday, October 13, 2012

Malawi yamfukuza balozi wa Tanzania nchini.humo


Yadaiwa amepewa saa 48 kuondoka



Balozi Patrick Tsere

Kuna taarifa ambazo bado hazijathibitishwa kutoka Ikulu ya Malawi kuwa. Malawi imeamua kumfukuza balozi wa Tanzania nchini Malawi Patrick Tsere.
 

Kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na gazeti la Malawi Voice la nchini  Malawi  Tsere amepewa saa 48 aondoke nchini Malawi.

Hatua ya kumfukuza balozi huyo unafuatia mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa baina ya Tanzania na Malawi.

Gazeti hilo linaripoti Malawi imechukua hatua ya kumfukuza balozi huyo kufuatia mahojiano aliyoyafanya na Radio Zodiak ambapo alisema kuwa Ziwa Malawi au Nyasa linamilikiwa nusu na Malawi na nusu ni sehemu ya Tanzania.

Hatua ya kumfukuza balozi zinakuja siku chache baada ya Rais wa Malawi Joyce Banda kutangaza nchi yake kujitoa katika mazungumzo baina ya Tanzania na Malawi kuhusu mpaka wa ziwa hilo.

Akiongea na waandishi wa habari mjini Lilongwe Bi Banda alisema nchi yake imeamua kujitoa katika mazungumzo hayo kwa vile Tanzania imepeleka wanajeshi wake kwenda kufanya doria na pia kuchapisha ramani inayoonyesha kuwa mpaka wa ziwa Nyasa au Malawi upo katikati ya ziwa.
Balozi Patric Tsere kushoto akizungumza na waziri  Mkuu wa Tanzania Mizengo  Pinda

Bi Banda aliilaumu Tanzania kwamba imekuwa kigeugeu kwenye mazungumzo hayo .

Hatua ya kufukuzwa kwa balozi  huyo wa Tanzania inakumbusha hatua kama hiyo ambayo ilichukuliwa wakati wa utawala wa Marehemu Bingu wa Mutharika ambaye alimfukuza Balozi wa Uingereza nchini humo.


2 comments:

oakleyses said...

chanel handbags, burberry outlet online, christian louboutin outlet, nike air max, oakley vault, tiffany and co jewelry, michael kors outlet online, michael kors handbags, burberry outlet online, ray ban sunglasses, michael kors outlet store, prada handbags, oakley sunglasses, kate spade outlet, christian louboutin shoes, michael kors outlet, longchamp handbags, christian louboutin, coach outlet store online, true religion outlet, louis vuitton outlet, longchamp outlet online, nike free, true religion, polo ralph lauren outlet, gucci handbags, louis vuitton handbags, coach outlet, louis vuitton outlet, prada outlet, nike air max, jordan shoes, nike outlet, polo ralph lauren, louis vuitton, longchamp outlet, red bottom shoes, tory burch outlet online, kate spade outlet online, michael kors outlet online, coach purses, ray ban outlet, michael kors outlet online, coach outlet, tiffany jewelry, cheap oakley sunglasses, louis vuitton outlet online

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans