Friday, October 19, 2012

Uamsho Zanzibar watoa tishio jipya

Polisi wakidhiti vurugu Zanzibar
Kundi linalojiita kundi la Uamsho huko Zanzibar ambalo limekuwa likiendesha vurugu limetoa tishio jingine baada ya kudai kwamba Sheikh wao ametekwa  huku wakitoa tishio kwamba Sheikh huyo akikutwa amekufa basi nao wataua Padri au Mchungaji.

Kundi hilo linaamini kwamba huenda Sheikh huyo amekamatwa na Polisi, lakini Jeshi la Polisi viwani Zanzinbar limekanusha kuwa halihusiki na wala halijui Sheikh huyo kwa sasa yuko wapi.

Kamshna wa Polisi Visiwani Zanzibar Musa Ali Musa amekiri kuwa Polisi imesikia tishio hilo la kundi hilo la uamsho.
" Nasi tumepata taarifa hizo kwamba wanatishia kwamba Sheikh wao akikutwa ameuawa nao wataua Padri au Askofu.  Lakini wanasema Polisi mwachie sasa sisi tutamwachiaje mtu ambaye hatunaye sisi. Sisi Polisi tumejipanga kuimarisha ulinzi  na vurugu zozote zitakazojitokeza" amesema.

Tayari askari polisi mmoja aliuawa majira ya usiku ambapo inasadikiwa aliuawa na kundi hilo jambo  linatishia usalama wa Zanzibar na hasa kwa viongozi wa dini ya Kikristo ambao wapo visiwani humo.   

Zinzibar hapakaliki siku ya tatu sasa