Sunday, October 14, 2012

Viongozi wa Kikristo walaani: Makanisa yaliyochomwa yafikia 7

Kanisa mojawapo lililochomwa moto na waislamu huko Mbagala
 Makanisa yaliyochomwa moto katika vurugu za waislamu huko Mbagala baada ya mtoto wa miaka 12 kukojolea quran yamefikia saba hadi sasa.

 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova aliyataja makanisa yaliyoharibiwa kutokana na vurugu hizo kuwa ni Kanisa la Agape lililopo Kibonde Maji, Kanisa la Wasabato, Mbagala Kizuiani na kwamba mali zenye thamani ya Sh8 milioni za kanisa hilo ziliharibiwa.

Kova aliyataja makanisa mengine yaliyoharibiwa kuwa ni Kanisa Katoliki la Kristo Mfalme, Mbagala Rangi Tatu ambako walivunja vioo na kuharibu madhabahu na Kanisa la Anglikana Mbagala Kizuiani lililoharibiwa madhabahu, ambayo thamani yake bado haijajulikana.

Waamuni wa dini ya kislamu wakati wa fujo hizo
Mengine ni Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbagala na Kanisa la TAG Shimo la Mchanga.

Katika makanisa hayo mawili waliharibu milango na kuchoma nyumba ya Mwekahazina wa kanisa  pamoja na nguo za kichungaji zilizokuwa ndani ya nyumba hiyo.

Kamanda Kova alifafanua kuwa hadi jana walikuwa wakiendelea na msako wa kuwabaini watu wengine waliohusika na tukio hilo, akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zilizo sahihi.
Kova alisema mtoto anayetuhumiwa kudhalilisha Quran hiyo, ambaye hadi sasa anashikiliwa na polisi, atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, kwa kuzingatia umri wake.
Aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati polisi wakifanya uchunguzi wa kina.

Kufuatia tukio hilo viongozi mbali mbali wa Dini ya Kikristo wamelaani na kuitaka serikali kuchukua hatua ili kudumisha amani na utulivu.
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la K ilutheri Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa alisema kuwa suala hilo limeleta hali ya wasiwasi na kuwaomba waumini wote wa kanisa hilo kuwa na moyo wa kusamehe.

“Yote yaliyotokea ni ya kumwachia Mungu na kuendelea kumtegemea,” alisema Malasusa

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Mchungaji Dk Leonard Mtaita alisema  kuwa jumuiya yake itatoa tamko baada ya kupokea taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wa makanisa yaliyochomwa moto.”

Viongozi wa makanisa hayo wamekwenda kuangalia uharibifu uliofanyika, watakapokutana na kutupa taarifa rasmi, ndiyo tutaweza kutoa msimamo wetu rasmi,” alisema Dk Mtaita.Hata hivyo, alisema jambo hilo linapaswa kuchunguzwa kwa makini, kwani ingawa limeanzia kwa watoto huenda kuna mkono wa watu wazima nyuma yake.

Mtaita alidai kuwa hilo siyo tukio la kwanza kutokea na kwamba, kuna historia ndefu ya vurugu zinazohusiana na imani za dini hivyo aliitaka Serikali kuwa makini katika kulishughulikia.

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde alisema alisema matukio kama hayo yanachangiwa na jamii kukosa uvumilivu na kuheshimiana katika imani zao.”Ni tukio la kusikitisha, jamii ina wajibu wa kujua jinsi ya kuishi tukiwa katika imani tofauti, tunapaswa kujenga maadili ya kuheshimiana dini zetu,” alisema Padri Makunde.

Aliongeza kuwa tukio hilo, ambalo limeanzia kwa watoto ni ishara kuwa jamii haijatekeleza wajibu wake katika kuwajengea watoto misingi ya kuheshimu imani za wengine.Alitahadharisha kuwa ikiwa jamii haitakuwa na busara na subira katika kupokea mambo watakayoona kuwa ni tofauti na imani zao, basi taifa liko katika hatari ya kuingia kwenye machafuko.“Kupokea mambo kwa jazba kuna athari sana, pamoja na amani tuliyoipata na kudumu nayo kwa zaidi ya miaka 50, inaweza kupotea ndani ya muda mfupi,” alisema Padri Makunde

2 comments:

oakleyses said...

chanel handbags, burberry outlet online, christian louboutin outlet, nike air max, oakley vault, tiffany and co jewelry, michael kors outlet online, michael kors handbags, burberry outlet online, ray ban sunglasses, michael kors outlet store, prada handbags, oakley sunglasses, kate spade outlet, christian louboutin shoes, michael kors outlet, longchamp handbags, christian louboutin, coach outlet store online, true religion outlet, louis vuitton outlet, longchamp outlet online, nike free, true religion, polo ralph lauren outlet, gucci handbags, louis vuitton handbags, coach outlet, louis vuitton outlet, prada outlet, nike air max, jordan shoes, nike outlet, polo ralph lauren, louis vuitton, longchamp outlet, red bottom shoes, tory burch outlet online, kate spade outlet online, michael kors outlet online, coach purses, ray ban outlet, michael kors outlet online, coach outlet, tiffany jewelry, cheap oakley sunglasses, louis vuitton outlet online

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans