Sunday, October 14, 2012

Watanzania wamkumbuka Nyerere na vurugu za kidini

Wasema enzi uongozi wake haya hayakuwepo
Hayati Julias Kambarage Nyerere Rais wa Kwanza wa  Tanzania enzi za uhai wake
Watanzania leo wanakumbuka kifo cha  baba yao wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere wakati nchi  ya Tanzania leo ikishuhudia vurugu za kidini ikiwemo kuchomwa kwa baadhi ya makanisa huko Zanzibar kutokana na kile kichodaiwa harakati za kukerwa na Muungano na tukio la Mbagala ambapo makanisa yamechomwa baada ya mtoto mwenye miaka 12 kukojolea quran.

"Nyerere alikemea kwa nguvu zote ubaguzi , udini  pamoja na ukabila na kuwafanya Watanzania wote wajihisi kuwa ni ndugu moja. Hata hivyo kinachosikitisha ni misingi hiyo aliyoiacha kuanza sasa kubomoka taratibu hadi leo tunashuhudia haya yaliyotokea Zanzibara na Mbagala".Anasema mwandishi mmoja maarufu.

 Amewataka viongozi waliopo madarakani kurejea tena misingi hiyo ambayo iliijenga taifa kwani katika uongozi wa Mwalimu matukio kama haya hayakuwepo hata kidogo maana alikuwa ni mkali kwa yoyote anaendekeza udini , ukabila au rangi.

"Labda viongozi wetu wamesahau misingi hiyo, kama ni kumuuenzi baba wa Taifa leo basi ni vyema viongozi wetu wakawa wakali na watu wanaoendekeza udini. Inawezekana kunyamaza kimya ndio sababu ya kutufikisha hapa tulipo. Kama viongozi wetu wangekuwa wakali tangu baada ya kusikia yaliyotokea huko Zanzibar kwa watu hao wanaolibomoa taifa labda leo tungezungumza mengine". Anafafanua.