Saturday, December 8, 2012

BREAKING NEWS!!! Habari zaidi kuhusu ajali ya Iringa leo zaidi ya 10 wafariki

Watu kumi wanasadikiwa kufariki dunia huko mkoani Iringa katika ajali ya basi barabara ya Iringa.
Hata bado kumekuwa na mgongano wa ukweli wa idadi ya watu waliofariki katika ajali hiyo kwani wakati duru za kiusalama  zikidai mtu mmoja tu ndiye aliyekufa , taarifa  kutoka kwa  mashuhuda wa ajali  hiyo pamoja na taarifa  zilizothibitishwa na diwani  wa kata  hiyo ya Mseke Robert Lawa alidai  kuwa  jumla ya maiti  watano   walikuwa  wametolewa hadi majira ya saa 10:45 jioni .
Diwani huyo anasema  jitihada za  kulivuta basi hilo kuwavuta abiria  waliobanwa na kuangalia maiti  wengine  zikiendelea na kukiri  kuwa kazi ya  uokoaji iliendelea  kuwa ngumu zaidi baada ya kutumia masaa zaidi ya mawili kuendelea kuwaokoa majeruhi na kuwakimbiza  Hospitali ya mkoa  wa Iringa. 


Hadi sasa taarifa zinasema miili ya watu 11 imeshatolewa kwenye basi hilo.
Mashuhuda  wa ajali  hiyo ambao  walipata  kuzungumza na mwandishi  wa habari  hizi kwa njia ya  simu leo  walisema  kuwa ajali  hiyo ilitokea majira ya saa 8 za mchana na  chanzo  cha ajali  hiyo ni kugoma  kuingia gia na kufeli kwa breki wakati likijaribu  kupanda mlima mdogo uliopo eneo  hilo pamoja na  ubovu  wa basi  hilo lenye namba za usajili  T 803 APV Nissani mali ya Msanya  Trans ambalo lilikuwa  likitoka mjini Iringa  kwenda Usokami  wilaya ya Mufindi .

John  Kalinga mmoja kati ya mashuhuda  wa tukio  hilo alisema  kuwa basi lilikuwa likielekea Usokami na baada ya  kufika katika  eneo la Kichakani  lilikosa mwelekeo kutokana na mwendo kasi ambao  dereva  wa basi  hiyo alikuwa akiendanao na hivyo kuyumba na  kupinduka .

Alisema  mara baada ya ajali  hiyo kutokea  abiria  wote  zaidi ya 50 walifunikwa na basi  hilo na kufanya wasamaria wema kufanya badiii kubwa kuokoa majeruhi hao ambao waliokuwa  wamefunikwa na basi hilo.

Kwa upande  wake mmoja kati ya majeruhi  wa ajali  hiyo alisema  kuwa basi  hilo ni bovu  ambapo  kila  wakati  askari wa usalama barabarani  wamekuwa  wakiliacha kuendelea na safari  jambo ambalo ni hatari kwa usalama  wa  wananchi  wanaotegemea usafiri  huo katika eneo  hilo la Usokami  wilaya ya Mufindi.