Saturday, December 22, 2012

Lema asubiriwa na Mapokezi Makubwa Arusha leo baada ya kushinda Rufaa

Godbless Lema akifurahi hapo jana baada ya kushinda rufaa na kurejeshewa ubunge wake

Mapokezi makubwa yanamsubiri Mbunge wa Arusha Mjini leo Godbless Lema ambapo Wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Arusha wanatarajiwa kumiminika kwa wingi kumlaki Mbunge huyo aliyeshinda rufaa hapo jana na kurudishiwa ubunge.

 Jana Mahakama ya Rufaa Tanzania ilitengua uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha iliyomvua ubunge huo Aprili 5, mwaka huu.



Lema alivuliwa ubunge na Jaji, Gabriel Rwakibarila baada ya kuridhika na ushahidi wa walalamikaji; Mussa Mkanga, Agnes Mollel na Happy Kivuyo pamoja na mashahidi wao kuwa alitumia lugha za kashfa na matusi dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk Batilda Burian.

Jopo la Majaji wa Rufaa, Bernard Luanda, Salum Massati na Nathalia Kimaro lilitengua hukumu ya Mahakama Kuu baada ya kuridhika kuwa hakukuwa na uthibitisho wowote kuwa wadai watatu katika shauri ya msingi ambao walikuwa wajibu rufaa, walikuwa wapigakura katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mengi yamezungumzwa kuhusu hukumu ya Jaji Rwakibarila na pengine yatazungumzwa kuhusu hukumu ya jana ya Jopo la Majaji wa Rufaa. Wapo wanaofurahi na waliochukizwa na hukumu zote mbili.

Hoja tatu zimezua mjadala baada ya hukumu ya Mahakama Kuu na pengine zitaendelea kujadiliwa hata baada ya hukumu ya jana. Kimsingi, hukumu iliyomrejesha Lema bungeni ambayo kwa njia moja au nyingine, imejibu maswali yaliyotawala katika medani ya sheria.

Hoja ya msingi iliyojibiwa na Mahakama ya Rufaa ni kuhusu haki ya wadai, Mkanga, Agnes na Kivuyo iwapo walikuwa na uhalali na haki ya kufungua madai mahakamani kulalamikia mambo ambayo hayakuathiri haki yao kama wapigakura.

Pili, ni Je, Jaji Rwakibarila alikuwa sahihi kukubali hoja za wadai na mashahidi wao ambao ni wanaCCM na kuyatumia kutengua ushindi wa Lema, lakini akatupilia mbali ushahidi wa utetezi kwa sababu mashahidi wote walikuwa ni wanachama na viongozi wa Chadema, hivyo walikuwa na masilahi kwa upande mwingine.

Wakati mdai wa pili, Mollel ni Mwenyekiti wa Mtaa kupitia tiketi ya CCM, yule wa tatu, Happy Kivuyo alikuwa Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Sokon I, jijini Arusha wakati mdai wa kwanza, Mussa Mkanga aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sombetini kwa zaidi ya miaka 15 kwa tiketi ya CCM.

Tatu, ilikuwa sahihi kisheria Mahakama kumvua Lema ubunge kwa ushahidi wa mdomo usio na nyaraka za kuthibitisha madai dhidi yake?

Katika uamuzi wa jana, Jopo la Majaji wa Rufaa walizingatia hoja moja tu ya wadai kutokuwa na haki kisheria kufungua malalamiko kwa mambo ambayo hayakuathiri haki zao za kupiga kura.

Katika uamuzi wao uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Elizabeth Mkwizu, Jopo hilo lilienda mbali kwa kusema hakukuwa na kumbukumbu zozote katika nyaraka za Mahakama zanazoonyesha kama kweli wadai hao ni wapigakura waliosajiliwa kwenye daftari la kudumu la wapigakura.

Tangu hatua za awali za usikilizwaji wa shauri hili, Wakili wa Lema, Method Kimomogolo na Wakili Mkuu wa Serikali, Timon Vitalis aliyekuwa akimwakilisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali walipinga uhalali wa wadai ya kufungua kesi kulalamikia masuala ambayo hayakuathiri haki yao ya kupiga kura.

2 comments:

oakleyses said...

ferragamo shoes, soccer shoes, nike roshe, nfl jerseys, vans outlet, jimmy choo shoes, beats headphones, reebok shoes, valentino shoes, lululemon outlet, birkin bag, p90x workout, ugg outlet, asics shoes, mac cosmetics, longchamp, hollister, mcm handbags, ugg, babyliss, marc jacobs outlet, north face jackets, insanity workout, celine handbags, soccer jerseys, uggs on sale, canada goose outlet, wedding dresses, uggs outlet, replica watches, uggs outlet, canada goose, nike huarache, north face jackets, ugg boots clearance, mont blanc pens, instyler ionic styler, herve leger, nike trainers, canada goose outlet, canada goose outlet, giuseppe zanotti, new balance outlet, bottega veneta, ghd, ugg boots, chi flat iron, abercrombie and fitch, ugg soldes

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans