Sunday, March 24, 2013

Nani kama Tanzania!!! yaibamiza Morocco 3 - 1, Je Safari Brazil imenukia?


Mshambuliaji wa Tanzania Thomas Ulimwengu akijaribu kuwatoka wachezaji wa Morocco katika uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kwa Tanzania imebamiza Morocco 3 -1 na kufufua matumaini ya kwenda kucheza kombe la dunia Brazil mwaka 2014.
Tanzania imefufua matumaini ya kucheza kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 kama mwendo wa ushindi utaendelea. Hii inafuatia kuichapa moja kati ya ngumu barani Afrika na ambayo iliwahi kushiriki mara kadhaa michuano ya kombe la dunia timu ya Morocco magoli 3 - 1. Kwa sasa kiwango cha Tanzania kinaonekana kupanda kwani katika siku za hivi karibuni ilichapa timu maarufu barani Afrika Cameroon na Zambia zilipokutana katika mechi ya kirafiki.

Kwa ushindi huo sasa Tanzania inashika nafasi ya pili katika kundi C ikiwa na pointi 6 baada ya kucheza mechi mechi  tatu ambapo mechi ya kwanza iliyochezwa Juni 10 mwaka jana  Tanzania iliifunga Gambia 2 -1 jijini Dar es Salaam na baadae  ilifungwa magoli 2 - 0 na Ivory Coast  ugenini.

Katika mechi nyingine ya C iliyochezwa hapo jana Ivory Coast imechabanga Gambia 3 -1 mjini Abidjan.na kuifanya Ivory iongoze kundi C ikiwa na point 7 huku Tanzania ikishika nafasi ya pili na pointi 6.

Tanzania itarudiana na Morroco June 7 mwaka huu nchini Morocco na baada ya wiki moja itamenyana Ivory Coast jijini Dar es Salaam June 14 mwaka huu.

Mechi ya Mwisho ambayo itaamua kama Tanzania itakwenda Brazil kusakata kambu kumbu katika fainali ya kombe la dunia itafanyika nchini Gambia Septemba 9 mwaka huu. Msimamo kamili wa Kundi C hadi jana huu hapa chini.



Group C
Team
MP
W
D
L
GF
GA
Pts
3
2
1
0
4
5
7
3
2
0
1
5
4
6
3
0
2
1
4
6
2
3
0
1
2
2
6
1




Score boad ikionyesha Tanzania imeifunga timu ngumu ya Morocco mabao 3 - 1. Je Tanzania imeanza safari ya kuelekea Brazil kwenye fainali ya kombe la dunia 

No comments: