Thursday, May 9, 2013

David Moyes kumrithi Ferguson Man United


Kocha Everton anatarajiwa wakati wowote kutajwa kumrithi Kocha wa muda mrefu wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye ametangaza kutaafu.
Sir Alex Ferguson








Tangazo la kumtangaza Davidi Moyes linatarijiwa kutolewa baadae leo na Klabu ya Manchester United.

Ferguson mwenye miaka 71 alitangaza nia yake ya kustaafu kuifundisha Manchester United hapo jana jumatano baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa miaka 27.

Mrithi wake mtarajiwa David Moyes mwenye 50, ambaye ni raia mwenzake wa Scotland ambaye ameifundisha Everton tangu mwaka 2002 alikuwa na mazungumzo hapo jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Manchester United, Bill Kenwright hapo jana jioni.

Baadae leo Moyes alitarajiwa kuwaaga wachezaji na wafanyakazi wa klabu ya Everton ambapo anatarajiwa kuwaeleza uamuzi wake wa kujiunga na Man United wakati watakapokutana katika mazoezi ya asubuhi.

Kocha wa Wigan Roberto Martinez na Michael Laudrup wa Swansea wanatajwa huenda wamrithi Moyes kuifundisha Eveton.

Hata hivyo Moyes anatarajiwa kuendelea kuiongoza Everton katika mechi yake ya mwisho katika uwanja Goodson Park  siku ya Jumapili baina ya Everton na West Ham.