Saturday, August 17, 2013

Je ni urafiki wa mashaka? Kikwete apokewa na Banda kwa furaha


Rais Jakaya Kikwete amewasili nchini Malawi katika mkutano wa Jumuiya ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC na kupokelewa kwa furaha na mwenyeji wake Rais wa Malawi Joyce Banda.

Tanzania na Malawi zinavutana kuhusu ziwa Nyasa au Malawi kama linavyojulikana huko Malawi.
Hata hivyo inaonekana kuna hali ya upendo baina ya nchi hizi mbili ambazo zimepakana na zina uhusiano wa kiistoria tangu zamani.

Katika mgogoro wa mpaka Malawi inasema Ziwa lote la Nyasa ni mali ya nchi hiyo huku Tanzania ikisema mpaka wa ziwa hilo upo katikati kama zinavyosema sheria za kimataifa kuhusu maji na bahari.

Wataalam wa masuala ya Siasa na Kidiplomasia wanaona mzozo baina ya Tanzania na Malawi ni sawa na ugomvi wa ndugu waliozaliwa tumbo moja ambao huonekana kama mkubwa lakini ndugu hao baadae hukaa pamoja. "Damu ni nzito kuliko maji! Wahenga walisema.

No comments: