Sunday, September 15, 2013

Padri aliyemwagiwa tindikali atua Dar kwa matibabu

Padri Joseph Mwang'amba akishuka kwenye ndege ya kukodi
Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Cheju, Mkoa wa Kusini Unguja, Joseph Mwang’amba aliyemwagiwa tindikali na watu wasiojulikana ameletwa Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Kiongozi huyo wa dini, aliyejeruhiwa maeneo ya usoni, mikononi na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali hiyo alisafirishwa jana na ndege ya kukodi ya Shirika la Coastal kutoka visiwani humo hadi Dar es Salaam na baadaye kupelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.


Katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Kiongozi huyo aliyewasili saa 4.16 asubuhi  aliongozana na Padri Thomas Assenga.

Kiongozi huyo alikuwa akitembea taratibu, huku akijitahidi kujifunika mwili wake na kanga kuzuia mwanga wa Jua kutokuathiri zaidi mwili wake ulioathiriwa na tindikali.
Wakati huo huo Rais wa Zanzibar Dk  Mohamed Shein alisema Polisi inatakiwa kuongeza nguvu za uchunguzi ili kukabiliana na matukio ya kikatili ya umwagaji wa tindikali, yanayoshamili visiwani humo hivi sasa.
“Hatuwezi kuviacha vitendo hivi viendelee … ni lazima Jeshi la Polisi lijitahidi kuwatafuta wahusika ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema Dk Shein.
Dk Sheni alisema, kitendo hicho ni cha kikatili na kisichovumilika na kuongeza kuwa wahusika lazima wasakwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kwa upande wake, Padri wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Zanzibar, Thomas Assenga aliyefuatana na kiongozi huyo mpaka MNH, alisema siku za nyuma Padri Mwang’amba alitolewa vitisho na mtu ambaye hamfahamu wakati akienda kutoa huduma katika kituo cha wazee cha Welezo.
Alisema kabla ya kufika kituoni hapo, kuna eneo ambalo nyakati za asubuhi watu hufanya mazoezi barabarani ambapo kuna mtu mmoja alimtolea maneno ya vitisho.
“Unajua kawaida ya watu wa Zanzibar hufanya mazoezi barabarani, sasa kipindi anapita eneo hilo katika kilima, kuna mtu alimwambia atamfanyia kitu kibaya ambacho hatujui ndiyo hiki au la,” alisema Padri Assenga na kuongeza:
Alisema Juni mwaka huu mara baada ya kupewa vitisho hivyo alikwenda kutoa taarifa kwa Sheha wa eneo hilo na kituo cha polisi.
“Mara baada ya kutolewa vitisho hivyo Juni mwaka huu, alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mkuu wa eneo hilo (Sheha) na kituo cha polisi.”
Aidha pia imebainika kuwa Padri huyo alitishiwa kuuawa miezi mitatu kabla ya kukutwa na tukio hilo.
Akielezea tukio la kumwagiwa tindikali Padri Mwang’amba, alisema alimwagiwa saa 9:45 alasiri juzi wakati akizungumza na simu nje ya internet cafĂ© iliyopo eneo la Mlandege.
Padri Assenga alisema kabla ya kumwagiwa tindikali, Padri huyo alikuwa ndani ya internet akitoa ‘photocopy’ za nyaraka. Alipokuwa akitoa ‘photocopy’ (nakala) alipigiwa simu na mtu ambaye anamfahamu hivyo ikabidi atoke nje kuongea naye, lakini alivyokuwa akiongea alimwona kijana akija na kikopo alichokishika mkononi na kummwagia na kukimbia kuelekea katika mitaa ya eneo hilo,” alisema Padri Aseenga.
Alisema mara baada ya hapo, alipelekwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, kwa matibabu baada ya kujeruhiwa usoni, kifuani na mikononi ambapo hivi sasa afya yake inaendelea vizuri.
Naye , Msemaji wa Jeshi la Polisi, Zanzibar Mohamed Muhina alisema, hana taarifa hizo za vitisho na kuahidi kulifanyia kazi.
“Tukio limetokea mchana kweupe na watu walikuwapo lakini wananchi wamekuwa hawatupi ushirikiano hivyo tunawaomba kutupa ushirikiano ili kukomesha vitendo hivi,” alisema Muhina.
Tukio lilivyokuwa
Akifafanua zaidi kuhusu tukio hilo, Padri Mwang’amba alisema kwamba lilitokea nje ya duka linalotoa huduma za mawasiliano ya mtandao (Sun Shine Internet Caffee) liliopo eneo la Mlandege Wilaya ya Mjini Unguja, ndipo alipotokea kijana mmoja na kumwagia tindikali.
Padri Mwang’amba akimweleza Dk Shein kuwa hali yake ni nzuri na anaweza kuona vizuri, lakini anatarajia kupata nafuu zaidi baada ya uvimbe kupungua katika sehemu za usoni na machoni mwake.
“Hali yangu ni nzuri lakini natarajia uvimbe ukipungua nitaona vizuri zaidi,” alisema Padri Mwang’amba na kuongeza kuwa ilikuwa ni bahati kwake kwa kutoathirika sana.


3 comments:

oakleyses said...

lululemon canada, ray ban pas cher, michael kors pas cher, burberry pas cher, sac vanessa bruno, north face, nike air force, hollister uk, coach outlet, abercrombie and fitch uk, nike air max uk, nike blazer pas cher, nike air max uk, new balance, coach outlet store online, nike roshe, true religion outlet, sac longchamp pas cher, timberland pas cher, true religion jeans, polo ralph lauren, mulberry uk, coach purses, true religion outlet, guess pas cher, nike tn, nike free run, sac hermes, michael kors, ray ban uk, hollister pas cher, north face uk, ralph lauren uk, nike air max, polo lacoste, converse pas cher, oakley pas cher, air max, replica handbags, true religion outlet, michael kors, kate spade, vans pas cher, michael kors outlet, louboutin pas cher, nike roshe run uk, hogan outlet, longchamp pas cher, jordan pas cher, nike free uk

oakleyses said...

nike air max, longchamp outlet, louis vuitton, nike outlet, prada handbags, ray ban sunglasses, jordan shoes, ugg boots, tiffany and co, ray ban sunglasses, polo outlet, nike free, christian louboutin outlet, louis vuitton, prada outlet, chanel handbags, ray ban sunglasses, christian louboutin uk, nike air max, longchamp outlet, louis vuitton outlet, tiffany jewelry, kate spade outlet, uggs on sale, oakley sunglasses, louis vuitton outlet, christian louboutin shoes, longchamp outlet, polo ralph lauren outlet online, gucci handbags, replica watches, replica watches, tory burch outlet, oakley sunglasses wholesale, ugg boots, oakley sunglasses, cheap oakley sunglasses, oakley sunglasses, christian louboutin, louis vuitton outlet

oakleyses said...

michael kors outlet online, michael kors outlet online, uggs outlet, uggs outlet, michael kors outlet online, michael kors outlet, michael kors outlet, burberry handbags, michael kors outlet online, burberry outlet