Sunday, October 14, 2012

Wakristo leo kufanya ibada makanisani kwa tahadhari

  Wataka vyombo vya ulinzi na usalama viimaarishe ulinzi makanisani


Kanisa mojawapo lilolochomwa wakati vurugu za waislamu Mbagala
Leo wakristo katika makanisa mbali mbali  jijini Dar es Salaam na maeneo mengine wanatarajiwa kuhudhuria makanisani kwenda kusali lakini  huenda wakafanya ibada hizo kwa tahadhari kubwa kufuatia vurugu zilizofanywa na waislamu ambao walichoma baadhi ya makanisa katika maeneo ya Mbagala kufuatia mtoto aliyedaiwa kukojolea quran.

Katika baadhi ya maeneo ya jijini baadhi ya wakristo ambao hawakupenda kutaja majina yao wamesema wamekuwa na wasi wasi kufuatia tukio hilo jambo ambalo linawatia hofu siku ya leo wakati watakapokuwa makanisani kwenye ibada ya jumapili.

Baadhi wamevitaka vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi wakati wakristo leo watakapokuwa kwenye ibada ili kuepusha tukio lolote litakalohatarisha maisha yao.

"Mimi nina wasi wasi kufuatia tukio la kuchoma makanisa baada ya mtoto kudaiwa kukojolea quran. Naogopa hata kwenda kanisani kusali lakini kwa kuwa mimi ni mkristo nitakwenda tu Mungu najua atatulinda sisi hatutegemei ulinzi kutoka kwa binadamu." Amesema muumini mmoja wa dini ya Kikristo.

2 comments: