Sunday, November 14, 2010

Arsenal yaitafuna Everton 2-1


Arsenal ilifanikiwa kuhimili kishindo cha dakika za mwisho kilichooneshwa na Everton waliokuwa wakitafuta bao la kusawazisha.

Hata hivyo hadi dakika 90 za mwisho Arsenal waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Bakari Sagna alikuwa wa kwanza kuipatia Arsenal bao la kuongoza baada ya kupokea pasi ya krosi kutoka kwa Andrei Arshavin, kabla ya mlinda mlango wa Arsenal Lukasz Fabianski kupangua shuti la Louis Saha ambalo lingekuwa bao la kusawazisha.

Kiungo na nahodha wa Arsenal Cesc Fabregas mara tu kilipoanza kipindi cha pili, aliipatia Arsenal bao la pili baada ya pasi na gonga murua kati yake na Marouane Chamakh, huku Fabianksi akiwa katika patashika nyingine ya kuokoa mikwaju kutoka kwa Jermain Beckford, Steven Pienaar na Saha.

Dakika za mwisho Everton ilichachaa na kuonekana wangepata bao wakati wowote na alikuwa Tim Cahill aliyefanikiwa kupachika bao la kufutia machozi katika dakika ya 89.
Kwa matokeo hayo Arsenal imerejea katika nafasi ya pili waliyoipoteza kwa Manchester United kwa muda sasa kwa kufikisha pointi 26 nyuma ya mabingwa watetezi Chelsea.

No comments: