Waambiwa wailipe moja kwa moja serikali ya Tanzania
Kampuni ya Uingereza ya kutengeneza zana za kivita BAE Systems imetakiwa na wabunge wa Uingereza kuilipa Tanzania fedha za fidia za mauzo ya rada zaidi dola milioni 30 haraka iwekanavyo.
Wabunge hao wameshambulia kampuni hiyo kwa kujihusisha na rushwa wakati wa mauzo ya rada hiyo hasa pale walipomlipa dalali zaidi ya dola milioni 12 ambazo haziwekwa kwenye vitabu vya mahesabu.
Hivi karibuni kampuni hiyo ilikuwa ikivutana na serikali ya Tanzania kuhusu njia ya kulipa fedha hizo ambapo ilikuwa ing'ang'nia kulipa fedha hizo kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali ya Uingereza huku serikali ya Tanzania ikipendekeza fedha hizo zilipwe moja kwa moja serikalini.
Sasa huenda ubishi huo ukamalizika kwani wabunge wa Uingereza wameitaka BAE kulipa serikali ya Tanzania fedha hizo moja kwa moja na isijifanye inajua namna ya kutumia fedha hizo kuliko serikali ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment