Monday, August 8, 2011

Tido, Warungu Mabosi wapya Al Jazeera

Tido asema sio kweli yeye ana mipango mingine


Television mpya ya kimataifa itakayotangaza kwa lugha ya Kiswahili ya Al Jazeera hatimaye imewanyakuwa magwiji wa utangazaji wa Afrika mashariki na kati waliowahi pia kufanya kazi katika shirika la Utangazaji la Uingereza BBC Tido Mhando na Joseph Warungu.

Makao makuu ya televisioni hiyo yatakuwa  mjini Nairobi nchini Kenya na inatarajiwa kuanza kurusha matangazo kwa lugha ya Kiswahili mwanzoni mwa mwaka 2012.


Tido Mhando

Kuna zaidi ya watazamaji na wasikilizaji wa lugha ya Kiswahili wapatao milioni 150 barani Afrika hata katika hatua za awali ataanza na maeneo machache kurusha matangazo hayo.


Tido na Warungu waliwahi kushika nyazifa mbali mbali katika shirika la Utangazaji la Uingereza ambapo Tido alikuwa ni Mhariri wa Idhaa ya Kiswahili wakati Warungu alikuwa ni Mhariri wa Afrika wa idhaa ya Kiingereza.

Katika hatua nyingine Tido Mhando amekana taarifa hizo na kusema sio za kweli kwani yeye ana mipango mingine na hana mpango wa kufanya kazi hiyo na wala hajawahi kuomba kuwa mmoja wa mabosi wa Al Jazeera.

Alaumu taarifa zilizosambazwa na mtandao wa The Jackal News  na kusema zimepotosha taarifa hizo kwa kuchapisha bila kuwasiliana naye.