Sunday, August 7, 2011

Wa Marekani waliomuua Osama wauawa Afghanistan


Wanajeshi 30 wa Marekani ambao baadhi yao ni wa kikosi maalum wameuawa na kikundi cha kigaidi cha Taliban baada helkopata yao kushambuliwa na makombara ya kundi hilo Mashariki mwa Afghanistan.

Makomandoo saba wa Afghanistan na mkalimani ambaye ni raia nao pia walikuwepo kwenye helkopta hiyo.

Vyanzo vya habari vya Jeshi la Marekani zinasema wanajeshi wengi wa kikosi hicho maalum ni kutoka jeshi la wanamaji wa Marekani ambacho ndicho kilichomuua aliyekuwa gaidi namba moja duniani Osama bin Laden.

Idadi ya wanajeshi wa kikosi cha wanamaji waliouawa ni ishirini.

Hili ni tukio la kubwa la wanajeshi wa Marekani kuuawa katika tukio moja tangu mgogoro wa Afghanistan ulipoanza.

Tayari idadi ya waliofariki wamethitishwa na Uongozi wa majeshi ya NATO yanayoongoza operationi nchini Afghanistan.

Helkopta hiyo ilitunguliwa mapema asubuhi siku ya jumamosi katika jimbo la Wardak imesema taarifa kutoka ofisi ya Rais wa Afghanistan Hamis Karzai.

Wanajeshi hao wanaelezwa kuwa walikuwa wakitoka katika operationi ya kijeshi ambapo inaelezwa kuwa katika operationi hiyo wataliban nane waliuawa.

Tayari rais wa Marekani  Barack Obama ametoa salamu za rambi rambi kwa ndugu na jamaa waliofiwa na wanajeshi hao na ameleza kushutushwa na tukio hilo.