Wawili waachiwa huru
Mahamaka ya Kimataifa ya uhalifu ya The Hague Uholanzi ICC imewakuta
washtakiwa wanne wa machafuko ya kiasa nchini Kenye kuwa wana kesi ya kujibu.
Naibu Waziri Mkuu Uhuru Kenyatta na Katibu wa Baraza la
Mawaziri Fransis Muthaura sasa watashtakiwa kwa makosa dhidi ya binadamu ikiwa
ni pamoja na makosa ya mauaji na utesaji.
Naye William Ruto na Joshua Arap Sang nao wamekutwa na
kesi ya kujibu kuhusu machafuko hayo
Waliachiwa huru kwa kukosa ushahidi wa kutosha ni Mkuu wa
Polisi wa zamani Mohamed Hussein Ali na Waziri wa Viwanda Hendry Kosgey.
Kenyatta ambaye alikuwa ni mfuasi wa Mwai Kibaki anadaiwa
alishiriki machafuko hayo yaliyosababisha vifo vya watu zaidi 1,200 kuwaua na kuwabaka wafuasi wa Raila Odinga.
No comments:
Post a Comment