. Aagiza uchunguzi ufanyike ukweli ujulikane
. Ataka madaktari wasitishe mgomo la sivyo watafukuzwa kazi
Katika hotuba yake ya Mwisho wa mwezi Rais Jakaya Kikwete aliayasema hayo soma hotuba kamilia hapa chini
Rais Jakaya Kikwete |
HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 30 JUNI, 2012
Ndugu Wananchi,
Kama
ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa
kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza nusu ya kwanza ya mwaka 2012
salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa kuzungumza nanyi kila mwisho wa
mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili. Jambo la kwanza ni suala la
usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili ni la mgomo wa
madaktari.
Usafirishaji Haramu wa
Binadamu Nchini
Ndugu Wananchi;
Bila
ya shaka mtakuwa mmezisikia taarifa za tukio la kushtusha na kuhuzunisha la
kukutwa maiti 43 za watu wasiojulikana, zilizotupwa katika kichaka
kilichopo kijiji cha Chitego, Wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma tarehe 26 Juni,
2012. Pamoja na maiti hao, walipatikana watu 84 wakiwa hai lakini
wote wakiwa wamedhoofu na baadhi yao
wakiwa mahututi. Hatua za haraka zilichukuliwa kuwasafirisha watu hao
hadi Dodoma ambapo wale waliokuwa mahututi
walifikishwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kwa
matibabu na wengine walihifadhiwa katika Kituo cha Kati cha Polisi, Dodoma. Maiti 22
zilipelekwa Dodoma
na 21 zilipelekwa Morogoro kuhifadhiwa.
Taarifa
zilizopatikana kutoka kwa wale walionusurika zimebainisha kuwa watu hao ni raia
wa Ethiopia ambao walikuwa
safarini kwenda Malawi
na baadaye Afrika ya Kusini ambako wangetengenezewa utaratibu wa kwenda kuishi
Marekani na Ulaya. Kwa mujibu wa maelezo yao,
safari yao
ilianza miezi mitano iliyopita. Mwezi mmoja waliutumia Ethiopia na miezi minne waliitumia Kenya kabla ya kuletwa Arusha ambako walipakiwa
kwenye lori na kuanza safari ya kuelekea Malawi lakini ikaishia
Chitego. Lori walilopanda lilikuwa limezibwa kabisa na hivyo kusababisha
vifo kwa kukosa hewa.
Tukio
la Chitego, Dodoma
la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea
hapa nchini. Kwa jumla, katika kipindi cha takriban miaka 10 sasa
kumekuwepo na tatizo kubwa la wahamiaji haramu kuingia nchini. Kwa mfano,
kati ya mwaka 2005 na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683
wamekamatwa. Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu
watu 1,500 tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa
makwao. Wengi wa watu hao wanatoka Ethiopia
na Somalia na baadhi kutoka Pakistan na Bangladesh.
Wahamiaji
haramu wamekuwa wanaingia nchini kwa kupitia njia zisizo rasmi. Wapo
wanaotumia nchi kavu hasa kupitia mikoa ya Mara, Arusha, Kilimanjaro na
Tanga. Na, wapo wanaopitia baharini kwa kutumia fukwe za Pemba, Unguja na za mikoa ya ukanda wa Pwani ya Tanzania
Bara yaani Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara.
Ndugu
Wananchi;
Kwa
mujibu wa kauli zao, watu hao wamekuwa wanaeleza kuwa hawaji nchini kuhamia
bali wao ni wapita njia tu. Wanaelekea Afrika ya Kusini ambako
wameahidiwa kuwa watatengenezewa mipango ya kuhamia Marekani na Ulaya.
Watu hao pia wamethibitisha kuwepo kwa watu maalum wanaojihusisha na usafiri
wao tangu nchi watokako na zote wanazopitia mpaka kule waendako. Aidha,
wamesema kuwa wao wanawalipa watu hao ili wawasafirishe na hakika si kiwango
kidogo. Kwa jumla ni kwamba hili si suala la uhamiaji haramu bali ni la
biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
Ndugu
Wananchi;
Kufuatia
vyombo vyetu vya usalama kuwa makini na watu wengi kukamatwa ndipo
wasafirishaji walipobuni njia za kuwasafirisha kama
mizigo. Makontena, malori yaliyofunikwa nyuma na matenki ya mafuta na ya
maji yamekuwa yanatumika kwa ajili hiyo. Usafiri wa aina hiyo ndiyo
uliosababisha vifo vilivyotokea Dodoma tarehe 26 Juni, 2012 na vya watu 21
vilivyotokea mwezi Desemba, 2011 Mkoani Morogoro, na vile vya watu 12
vilivyotokea katika matukio mawili ya Mkoa wa Mbeya, mwezi Mei, 2012.
Ndugu
Wananchi;
Tarehe
27 Juni, 2012 nilikutana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini
kuzungumzia tukio la Chitego na suala zima la biashara hii haramu na hasa mbinu
mpya inayotumiwa na wasafarishaji. Nilitoa pongezi kwa vyombo vya dola
kwa kazi nzuri waifanyayo kudhibiti shughuli za biashara hii haramu hapa
nchini. Tulielewana kuwa waendelee kuimarisha udhibiti huo kwa lengo la
kukomesha kabisa biashara hii.
Niliagiza
pia kwamba kikundi kazi nilichokiunda mwaka 2006 kushughulikia ujambazi sasa
kielekeze sehemu ya nguvu zake kukabili tatizo hili. Aidha, kwa pamoja
tulikubaliana kuwa nchi yetu ishirikiane na wenzetu wa Ethiopia, Kenya,
Malawi,
Msumbiji na Afrika ya Kusini kutambua mawakala na kuwabana kwa mujibu wa
sheria. Tayari nimeshaanza kufanya mawasiliano na baadhi ya Wakuu wa Nchi
hizo kuhusu ushirikiano huo. Nashukuru wote wameafiki nchi zetu
zishirikiane kwa pamoja kuvunja mtandao huu mchafu na kutokomeza biashara hii
haramu na inayodhalilisha utu wa mwanadamu.
Ndugu
Wananchi;
Napenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru wenzetu, wakazi wa vijiji vya Chitego na Mkoka
kwa kazi nzuri walioifanya. Kwa kweli, wenzetu wameonesha uzalendo wa hali ya
juu kwa kutoa taarifa mapema juu ya jambo lenyewe, lakini pia wameonesha utu
kwa kuwajali wageni waliokumbwa na janga hili. Naushukuru pia uongozi wa Mkoa
wa Dodoma na Morogoro ikiwa ni pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kwa
kulishughulikia tatizo hilo kwa umakini mkubwa. Nimefurahishwa sana na ushirikiano
ulioonyeshwa na vyombo na taasisi mbalimbali za Serikali katika kushughulikia
suala hili.
Mgomo
wa Madaktari
Ndugu
Wananchi;
Jambo la pili ni kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa.
Nilipozungumza na Wazee wa Dar es Salaam katika Ukumbi wa Diamond Jubilee
tarehe 12 Machi, 2012, kuhusu mgomo wa Madaktari uliokuwa unaendelea wakati ule
pamoja na kuelezea chimbuko la mgomo na hatua iliyokuwa imefikiwa, nilielezea
mazungumzo yangu na viongozi wa Chama cha Madakari wakiwemo pia viongozi wa
Jumuiya ya Madaktari. Nilitoa taarifa kuwa tumeelewana kuwa watasitisha
mgomo na watarudi kwenye meza ya majadiliano na Serikali. Siku ile pia
nilielezea matumaini yangu kuwa mgomo ule utakuwa wa mwisho katika nchi
yetu. Bahati mbaya matumaini yangu hayo hayakuwa na hivi sasa
tunashuhudia tena wagonjwa wakiteseka, kuhangaika na wengine kufa kwa sababu ya
kukosa huduma wanazostahili kwa vile madaktari wao wamegoma tena.
Ndugu
Wananchi;
Kama
walivyoniahidi, madaktari waliacha kugoma na viongozi wao walirudi kwenye
mazungumzo na Serikali. Kama
ilivyoagizwa na Mahakama Kuu, Kitengo cha Kazi tarehe 8 Machi, 2012, kwa mujibu
wa Sheria ya Mahusiano Kazini, Namba 6 ya mwaka 2004. Chama cha
Madaktari na Serikali walifika katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (Commission
for Mediation and Arbitration) kwa ajili ya majadiliano. Kwa pamoja na
kwa ridhaa yao wote, pande hizo mbili ziliiomba
Tume hiyo iwape fursa ya kuzungumza wao wenyewe na wakimaliza mazungumzo
wataenda kusajili makubaliano yao.
Tume ikawakubalia. Ni vizuri ikakumbukwa kuwa siku ile ya tarehe 8 Machi,
2012 Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ilitoa zuio la mgomo pamoja na kuagiza
kuwepo mazungumzo baina ya pande mbili.
Ndugu
Wananchi;
Kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012,
vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha
Madaktari. Katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari
yalizungumzwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo:
1. Posho ya kuitwa kazini (on call allowance) iwe
asilimia 10 ya mshahara.
2. Posho ya kufanya kazi katika mazingira
hatarishi (Risk allowance) iwe asilimia 30 ya mshahara.
3. Madaktari wapatiwe nyumba grade A au posho ya
makazi ambayo iwe asilimia 30 ya mshahara.
4. Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu
iwe asilimia 40 ya mshahara.
5. Madaktari walipwe posho ya usafiri ya asilimia
10 ya mshahara au wakopeshwe magari.
6. Madaktari wanaoanza kazi walipwe mshahara wa shilingi
3,500,00/= kwa mwezi.
7. Madaktari wapatiwe Green Card za Bima ya afya.
8. Hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya
Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
9. Viongozi wa Kisiasa kulazimisha kupewa rufaa
nje.
10.
Madaktari
waliofukuzwa warudishwe kazini.
11.
Huduma za
afya ziboreshwe nchini.
12.
Posho ya
uchunguzi wa maiti iongezwe.
Ndugu
Wananchi;
Katika mambo hayo 12 pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana
wa pamoja kwa mambo saba. La kwanza, ni kuhusu usafiri wa kwenda
na kurudi kazini. Serikali ilieleza kuwa upo utaratibu kwa mujibu wa
Waraka wa Utumishi wa Serikali Na. 3 wa mwaka 2011 wa kuwakopesha wafanyakazi
wa Serikali fedha za kununulia magari au pikipiki, samani na matengenezo ya
magari. Ilikubaliwa kuwa madaktari waitumie fursa hiyo.
Jambo la pili, ni kuhusu madaktari kupatiwa Green Card za Bima ya
Afya. Jambo hili lilikubaliwa na Serikali na Wizara ya Afya
imekwishachukua hatua za utekelezaji wake.
Jambo la tatu, ni kuhusu hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi ya
Watendaji Wakuu wa Wizara ya Afya. Kwa pamoja walikubaliana kuwa suala hilo liko nje ya mamlaka ya Kamati yao ya pamoja, waziachie mamlaka husika za
uteuzi. Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi mpya.
Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka waonane
kuzungumzia hoja walikataa kumuona. Kwanza
walisema hawaoni sababu kwa vile wameyazungumza na Kamati yake kwa miezi mitatu
bila ya mafanikio
Jambo la nne walilokubaliana ni kuhusu viongozi kulazimisha kupewa rufaa
ya kutibiwa nje. Walikubaliana mambo mawili. Kwanza,
kwamba maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda kuwa madaktari wazingatie
maadili ya kazi zao na kukataa kutoa rufaa kwa mtu asiyestahili awe kiongozi au
asiwe kiongozi. Pili, walikubaliana kuwa hospitali zilizopo ziboreshwe
ili viongozi watibiwe hapa nchini. Ukweli ni kwamba kufanya hivyo ndiyo
sera ya Serikali. Nililieleza hili mwezi Desemba 30, 2005 katika hotuba
yangu ya kuzindua Bunge baada ya kuchaguliwa kwa mara ya kwanza kuongoza nchi
yetu.
Tumeiongeza sana
bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi
trilioni 1.2 mwaka 2011/12 na imekuwa ya tatu baada ya miundombinu na
elimu. Tumeziimarisha hospitali za Mikoa kwa vifaa tiba na wataalamu wa
afya. Kazi inaendelea katika hospitali za Wilaya. Tumewekeza katika
Hospitali ya Muhimbili. Hospitali hiyo ilivyo leo sivyo ilivyokuwa miaka
sita nyuma. Na kazi inaendelea hasa katika maeneo ambayo tunapeleka
wagonjwa nje. Matunda yake yanaanza kuonekana kwa upande wa figo, moyo,
kinywa na mipango inaendelea kwa upande wa ubongo na mishipa ya fahamu.
Tunaendelea kuimarisha mafunzo ya madaktari na madaktari bingwa, yote kwa
nia hiyo hiyo. Hivi sasa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba,Muhimbili
kinachukua wanafunzi wengi zaidi ya ilivyokuwa siku za nyuma na makazi mapya ya
chuo yanaendelea kuandaliwa ili kuchukua wanafunzi wengi zaid.
Mwaka 2005 tulikuwa na madaktari bingwa 46 mwaka huu tunao 520.
Ndugu
Wananchi;
Jambo la tano ambalo pande zote mbili zilikubaliana ni kuhusu madaktari
waliofukuzwa. Hawa ni wale Interns waliokuwa wamerudishwa Wizarani
kutoka Muhimbili na kupangiwa hospitali za Temeke, Ilala, Mwananyamala na
Lugalo. Hili ni jambo ambalo lilikuwa limemalizika kitambo na wote
walikuwa wamerudi Muhimbili.
Jambo la sita ni kuhusu mapendekezo mbalimbali yaliyotolewa na madaktari
kuhusu kuboresha huduma ya afya. Mapendekezo hayo yalihusu kutathmini
sera na mpango wa afya ya msingi, bajeti ya afya kuwa asilimia 15 ya
bajeti ya Serikali, kuwepo na utaratibu mzuri wa kuajiri madaktari na kuboresha
viwango vya ubora wa madaktari na kadhalika. Serikali imeyaafiki
mapendekezo hayo na yatafanyiwa kazi.
Jambo la saba, ambalo pande zote walilokubaliana ni kuhusu kuongeza
posho ya uchunguzi wa maiti. Hili ni jambo jipya halikuwepo
mwazoni. Hata hivyo, Serikali imelikubali na posho hiyo imeongezwa kutoka
shilingi 10,000/= hadi kufikia shilingi 100,000/= kwa daktari na shilingi
50,000/= kwa wasaidizi wake.
Ndugu
Wananchi;
Kuna masuala matatu ambayo yamekuwa na muafaka kwa kiasi fulani na
kutoafikiana kwa baadhi ya mambo. La kwanza ni suala la kufanya
kazi katika mazingira hatarishi. Serikali imekubali hoja ya kuchukua
hatua ya kuwalinda madaktari wanaofanya kazi katika mazingira hatarishi.
Serikali iliwaeleza kuwa watumishi wa kada zote za afya watapatiwa chanjo dhidi
ya maambukizi ya Hepatitis B na fedha zimetengwa katika bajeti ya
2012/13.
Aidha, Serikali imeeleza dhamira ya kurudisha posho ya
mazingira hatarishi kwa watumishi wa umma wanaostahili. Utekelezaji wake
utafanyika baada ya uchambuzi wa kina wa kubainisha mazingira hatarishi ni
yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike. Madaktari wamekataa
hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama
wanavyotaka wao, yaani asilimia 30 ya mshahara na kianze mara moja.
Jambo la pili ambalo wamekubaliana nusu nusu ni kuhusu nyumba za kuishi.
Serikali imekiri wajibu wake wa kuwapatia madakari nyumba za kuishi.
Aidha, imeeleza mpango ulioanza wa kujenga nyumba 700 za madaktari kote
nchini na kwamba hivi sasa ujenzi wa nyumba 90 unaendelea, 50
katika mkoa wa Mtwara na 40 katika mkoa wa Rukwa.
Kwa maeneo ambayo madaktari wanalipwa posho ya pango
Serikali imesema waajiri wataendelea kufanya hivyo kwa mujibu wa taratibu
zilizopo kwa watumishi wa umma wenye stahili ya kupewa nyumba. Jambo hilo limekataliwa na Madakari na kutaka lazima walipwe asilimia
30 ya mshahara kama posho ya nyumba.
Serikali kwa upande wake imeona vigumu kufanya hivyo na kuwasihi wakubali
wanayotendewa wafanyakazi wengine wote wa umma.
Jambo lingine ambalo lilikuwa na makubaliano ya nusu nusu ni kuhusu
posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu. Pande zote mbili
ziliafikiana kuwa yapo baadhi ya maeneo nchini yanayo mazingira magumu kwa
watumishi wa umma hivyo hatua zichukuliwe kuwasaidia watumishi hao.
Serikali imekubali wajibu wa kuweka utaratibu wa kuboresha maisha ya watumishi
katika maeneo hayo. Kwa ajili hiyo, Serikali itatoa mwongozo kwa mamlaka
za ajira kuhusu namna ya kuwasaidia watumishi hao kupunguza makali ya maisha
katika kila eneo badala ya kutegemea posho peke yake.
Kuhusu posho, Serikali imeeleza kuafiki kuwepo
posho ya aina hiyo ila itatekelezwa baada ya kufanya uchambuzi wa kuainisha
mazingira husika, kutambua watumishi waliopo na gharama zake.
Madaktari hawajakubali kusubiri zoezi la uchambuzi lifanyike, wanataka Serikali
ilipe posho hiyo sasa. Tofauti hapa si posho hiyo kuwepo, bali ni rai ya
Serikali ya kubaini maeneo yenyewe na kupanga aina ya hatua na viwango vya
posho kulingana na mazingira halisi ya maeneo. Madaktari hawaoni haja ya
kufanya hayo.
Ndugu
Wananchi;
Mambo mawili hayakuwa na muafaka kabisa kati ya pande zetu mbili. Jambo
la kwanza ni posho ya kuitwa kazini (on call allowance). Kwanza sina budi kueleza kuwa Serikali imekubali kuongeza
posho hiyo. Tangu Februari, 2012 posho iliongezwa kutoka shilingi
10,000/= hadi shilingi 25,000/= kwa daktari bingwa (Specialist), shilingi
20,000/= kwa dakari mwenye usajili wa kudumu (Registrars) na shilingi
15,000/= kwa madaktari waliohitimu ambao wapo katika kipindi cha mafunzo
kazini (Interns). Viwango hivyo vya posho vinatumika hivi sasa.
Madaktari kwa upande wao hawakukubali uamuzi huo wa
Serikali na kusisitiza walipwe asilimia 10 ya mshahara. Ugumu wa
kukubali pendekezo la madakari ni kuwa sharti la malipo haya ni mtu kuitwa
kazini. Ukitaka ilipwe kiwango cha mshahara ina maana kuwa hata kama daktari hakupangwa kuitwa au alipangwa na hakutokea
aendelee kulipwa. Hili haliwezi kuwa sahihi kufanya. Linaweza
kuwafanya baadhi ya madaktari kutokutimiza wajibu wao kwa vile wana hakika
mwisho wa mwezi malipo yako pale pale.
Ndugu
Wananchi;
Jambo la pili ambalo muafaka haukufikiwa baina ya Serikali
na madaktari ni kuhusu mshahara wa kuanzia kazi wa daktari. Madaktari
wanataka uwe shilingi 3,500,000/= wakati Serikali inasema kiasi hicho
hatukiwezi. Serikali imeeleza utayari wake wa kuongeza mshahara kwa kati
ya asilimia 15 mpaka 20 kama
ambavyo itafanya kwa watumishi wote wa umma katika mwaka huu wa fedha.
Kwa kiwango cha sasa cha mshahara wao, daktari ataanzia kati ya shilingi
1,100,000/= na 1,200,000/= kutegemea kiwango kipi hatimaye
kitaamuliwa. Madaktari wamekataa katakata na wameng’ang’ania shilingi 3,500,000/=.
Ndugu
Wananchi;
Huo ndiyo mlolongo wa mambo yaliyozungumzwa na pande zote
mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe. Katika kikao cha sita kilichofanyika
tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha Madaktari ulisema kuwa kwa vile hoja
ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko hawakuona haja ya kuendelea na
majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao. Waliahidi kutoa taarifa
ndani ya wiki mbili. Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT aliandika barua
kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano kwa upande wa
Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi waliopewa kutoka
Serikalini kwa ujumla wake.
Ndugu
Wananchi;
Baada ya majibu yale ya madaktari, tarehe 19 Juni,
2012, Serikali na Madaktari walikwenda kwa Msuluhishi (CMA) kutoa taarifa kuwa
mgogoro umekosa usuluhishi kama sheria
inavyotaka. Kwa pamoja pande zote mbili zilikubaliana suala hilo lifikishwe Mahakama
Kuu Kitengo cha Kazi. Wakati pande zote zinasuburi mgogoro huu kufikishwa
ngazi hiyo ya juu, upande wa Madaktari ukatangaza kuwepo kwa mgomo kuanzia saa
sita ya usiku tarehe 23 Juni, 2012. Hatua hiyo haikustahili kwani suala
lenyewe halijafika mwisho wa kushughulikiwa kwa mujibu wa Sheria za Mahusiano
ya Kazi nchini.
Ndugu
Wananchi;
Tarehe 22 Juni, 2012, Mwanasheria Mkuu wa Serikali akaenda
Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi kulifikisha suala la tishio la mgomo na kuomba
zuio la muda kufanywa. Mahakama Kuu ilikubali ombi hilo na kuagiza kuwa mgomo usitishwe.
Juhudi za kumtafuta Rais wa MAT, Dkt. Namala Mkopi na viongozi wengine wa MAT
hazikufanikiwa, Ofisi ya MAT ilikuwa imefungwa na simu zote za viongozi wa MAT
zilikuwa zimezimwa. Hatimaye tarehe 25 Juni, 2012, alipatikana na kupewa
amri hiyo ya Mahakama. Tarehe 26 Juni, 2012, Dkt. Mkopi alifika
Mahakamani ambapo alikana kuwa yeye hahusiki na kuitisha huo mgomo lakini
hakumtaja aliyehusika. Pamoja na rai hiyo, Jaji alimuamuru Rais wa MAT
akawatangazie wanachama wake kusitisha mgomo. Dkt. Namala Mkopi
hajafanya hivyo hadi leo na mgomo umekuwa unaendelea kinyume cha Sheria.
Ndugu
Wananchi;
Wagonjwa wanateseka na wengine kupoteza maisha kwa mgomo
huu usiokuwa halali kisheria ambao pia haustahili kuwepo hata kwa mujibu wa
maadili ya udaktari. Viongozi wa MAT na wenzao wanawaingiza
Madaktari katika mgogoro na Mahakama na waajiri wao isivyostahili. Ni
vyema viongozi wa Madaktari na madaktari wakatambua kuwa wanashiriki katika
mgomo usiokuwa halali ambao pia kiongozi wao mkuu amekana Mahakamani kuwa
hahusiki nao. Madaktari lazima watambue pia kwamba ajira zao wanaziweka
hatarini. Mfanyakazi ana kinga ya kutofukuzwa kazi na mwajiri kwa
kushiriki mgomo unaokubalika kisheria. Huu siyo. Watapoteza ajira,
hawana pa kukimbilia, hawana cha kiwalinda. Kwa madaktari interns,
wanahatarisha maisha yao
kwani hawatapata cheti cha kudumu wakishiriki mgomo usiokuwa
halali. Lazima watafakari sana
kwa hayo wafanyayo.
Ndugu
Wananchi;
Napenda kurudia maneno niliyoyasema tarehe 12 Machi, 2012, kuwa kuboresha
mishahara na maslahi ya wafanyakazi ni Sera ya Serikali yetu kwa maelekezo ya
Ilani ya Chama Tawala (CCM). Tumeitekeleza kwa vitendo sera hiyo, hata
hivyo ni ukweli ulio wazi kuwa nia yangu njema tu pekee haitoshi, lazima uwezo
wa kufanya hivyo uwepo. Kwa kulingana na uwezo uliopo, tumeendelea
kuboresha mishahara na maslahi ya wafanyakazi hatua kwa hatua tangu tuingie
madarakani. Tumefanya hivyo kwa jumla kwa wafanyakazi wote na kwa kada
mbalimbali za watumishi wa umma.
Miongoni mwa wafanyakazi wa umma walionufaika na hatua
hizo za Serikali ni madaktari na watumishi wa kada nyingine za huduma ya
afya. Tena nadiriki kusema madaktari tumewapa upendeleo mkubwa kuliko
watumishi wengine wa umma. Upendeleo upo kwenye mafunzo ambapo wanafunzi
wa udaktari wanagharimiwa na Serikali kwa asilimia mia moja wakati wanafunzi
wenzao wa taaluma nyingine hawako hivyo.
Ndugu
Wananchi;
Mwaka 2004/2005, mshahara wa kuanzia wa daktari ulikuwa
shilingi 178,700/=, mwaka 2005/ 2006 tuliupandisha na kuwa shilingi 403,120/=.
Tuliendelea kuupandisha mwaka hadi mwaka mpaka kufikia shilingi 957,700/=
wanazolipwa sasa. Kiasi hicho ni mara mbili ya mishahara ya watumishi wa
taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani hupata
shilingi 446,100/=.
Tunafanya hivyo kwa kutambua na kuthamini nafasi maalum ya
madaktari katika jamii na ukweli kwamba bado tunayo safari ndefu ya kuziba
pengo la madaktari nchini. Lakini inaonekana juhudi zetu zote hizo
hazithaminiwi.
Ndugu
Wananchi;
Sina budi kusisitiza kwamba tunapofanya hivyo
tunaongozwa na uwezo tulio nao wa kulipa. Kwa sasa hatuwezi
kuwaahidi kuwa tunao uwezo wa kuwalipa mshahara wa kuanzia wa shilingi 3,500,000/=
na posho zote zile. Tukifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa
shilingi 7,700,000/=. Kwa hakika kiasi hicho hatutakiweza. Si
vyema kutoa ahadi hewa kwa watu tunaowaheshimu na kuwathamini kama
walivyo madaktari.
Kutokana na ukweli huo basi kama
daktari anayeona kuwa hawezi kufanya kazi Serikalini bila ya kulipwa mshahara
huo awe huru kuacha kazi na kwenda kwa muajiri anayeweza kumlipa kiasi
hicho. Nasi tutamtakia kila la heri. Hana sababu ya kugoma ili
ashinikize kulipwa mshahara huo. Asisumbuke, hatalipwa mshahara huo.
Isitoshe, hana sababu ya kuendelea kuwa na mgogoro na mwajiri ambaye hana uwezo
wa kumlipa anachokitaka. Huna sababu ya kumpa usumbufu mwajiri wa
kukuandikia barua ya kujieleza au kukuachisha kazi. Kwa nini upate
usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa
kuachishwa kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa
24. Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo,
mwajiri anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na
sheria za kazi na maadili ya kazi ya udaktari.
Mamlaka za ajira zimeanza kuchukua hatua hizo na
wataendelea kufanya hivyo kwa wote wanaoendelea kugoma. Najua baada
ya hatua hizo kuchukuliwa kuna manun’guniko ya kuonewa. Hivyo, mlitegemea
mwajiri afanyeje? Ni bora kufanya hivyo ili ajue hana daktari aweze kufanya
utaratibu wa kuziba hilo
pengo na huyo ajae awe na mahali pa kuishi. Vinginevyo atakuwa anajidanganya
kuwa anae daktari ambae hayupo kazini na wala hataki kufanya kazi.
Ndugu
Wananchi;
Napenda kuwathibitishia kwamba dhamira ya Serikali ya
kuboresha maslahi ya watumishi wa umma wakiwemo madaktari iko wazi.
Tumekuwa tunafanya hivyo, na tutaendelea kufanya hivyo kulingana na uwezo wa
kibajeti. Ni vyema watumishi wa umma wakatambua kuwa hatuwezi kutumia
fedha zote au kiasi kikubwa mno cha pesa za umma kulipana mishahara.
Tukifanya hivyo, Serikali itashindwa kutoa huduma muhimu kwa wananchi ambao
ndiyo wengi na wanastahili kuhudumiwa. Hata hizo huduma za afya
tunazosema ni duni tuziboreshe, hatutaweza kuziboresha kama
tutatumia sehemu kubwa ya pesa za Serikali kuwalipa mishahara
wafanyakazi.
Hivi sasa matumizi ya mishahara ni asilimia 48 ya
bajeti ya Serikali. Kiwango hicho ni kikubwa mno. Uwiano mzuri ni
kuwa na matumizi ya mishahara yasiyozidi asilimia 35 ya bajeti na asilimia
65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi
na taifa. Sisi tumezidi kwa asilimia 13. Hivyo, hatuna budi
tukubali kujinyima kwa manufaa ya walio wengi.
Suala la Dkt. Steven Ulimboka
Ndugu
Wananchi;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu, napenda kuungana na
Watanzania wenzangu wote kuelezea masikitiko yangu makubwa na kuhuzunishwa
kwangu na kitendo cha kinyama alichofanyiwa Dkt. Steven Ulimboka usiku wa
tarehe 26 Juni, 2012. Kitendo hicho ni kinyume kabisa na mila na desturi zetu.
Watanzania hatujayazoea mambo hayo. Nimeelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na
usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane. Nimesema kuwa
ningependa ukweli huo ujulikane mapema ili tuondoe wingu baya la kutiliana
shaka na kulaumiana kunakoendelea hivi sasa.
Natambua kuwa Serikali nayo inatajwa katika orodha ya
wanaotiliwa shaka. Mimi nimeshangazwa sana na hisia hizo kwani siioni sababu ya
Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu
katika mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si
mtumishi wa Serikali, hivyo hakustahili kuwa sehemu ya majadiliano haya.
Kulikuwa na rai ya kutaka asiwepo, lakini nilisema wamuache maadam Madaktari
wanamuamini kuwa anaweza kuwasemea vizuri zaidi kuliko wao wenyewe walioajiriwa
na Serikali.
Ndugu
Wananchi;
Kama
nilivyoeleza, mazungumzo yalienda vizuri na mafanikio makubwa
yamepatikana. Yapo maeneo machache na hasa eneo la mshahara ambalo
hatukuweza kukubaliana. Hapo tulipofikia si pabaya na tulikubaliana sote
kurudi kwenye mkondo wa Sheria kusaidiwa. Kwa nini Serikali imdhuru Dkt.
Ulimboka? Na, kuhusu mgomo, Mahakama Kuu imekwishatoa amri ya kusitisha
mgomo. Anayekaidi amri ya Mahakama ananunua ugomvi na mhimili huo wa dola
ambao wenyewe una mamlaka ya kumtia adabu mtu huyo. Hivi baada ya kufika
hapo Serikali iwe na ugomvi na Dkt. Steven Ulimboka kwa sababu ipi na jambo
lipi hata iamue kumdhuru? Kama kuna mtu
wa Serikali kafanya, itakuwa kwa sababu zake binafsi na siyo za Serikali au kwa
kutumwa na Serikali.
Ndugu
Wananchi;
Kwa
niaba yangu na kwa niaba ya Serikali natoa mkono wa pole kwa Dkt. Steven
Ulimboka na kumuombea apone haraka ili aungane na familia yake na Watanzania
wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na
kumpongeza Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua
alizochukua za kumsaidia Dkt. Ulimboka.
Naomba
kumaliza kwa kuwasihi madaktari kuacha mgomo na kurejea kazini.
Watanzania wenzenu wanateseka na kupoteza maisha. Muwe na moyo wa huruma
na upendo na msaada kwa wagonjwa kama kiapo
chenu kinavyowataka.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!
Asanteni kwa
Kunisikiliza
Ndugu
Wananchi,
Kama ilivyo ada naomba nianze kwa kumshukuru
Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kumaliza
nusu ya kwanza ya mwaka 2012 salama. Kwa kutumia utaratibu wetu wa
kuzungumza nanyi kila mwisho wa mwezi, leo napenda kuzungumzia mambo mawili.
Jambo la kwanza ni suala la usafirishaji haramu wa binadamu nchini na la pili
ni la mgomo wa madaktari.
Usafirishaji
Haramu wa Binadamu Nchini

kati ya mwaka 2005 na hivi sasa jumla ya wahamiaji haramu 19,683 wamekamatwa.
Karibu wote wameshaondoshwa nchini na hivi sasa wapo karibu watu 1,500
tu magerezani wanaotumikia adhabu na kusubiri kurejeshwa makwao. Wengi wa
watu hao wanatoka Ethiopia

Tume hiyo iwape fursa ya kuzungumza wao wenyewe na wakimaliza mazungumzo wataenda
kusajili makubaliano yao.

uteuzi. Uongozi wa juu wa Wizara umebadilishwa na sasa kuna uongozi
mpya. Lakini, jambo la kustaajanisha hata Waziri mpya wa Afya alipowataka
waonane kuzungumzia hoja walikataa kumuona. Kwanza

yepi, viwango stahiki viwe vipi na nani hasa wahusike. Madaktari
wamekataa hili la kufanya uchambuzi, wanataka kiwango kiwe kama

mbili na matokeo ya mazungumzo yenyewe. Katika kikao cha sita
kilichofanyika tarehe 30 Mei, 2012, upande wa Chama cha Madaktari ulisema kuwa
kwa vile hoja ya nyongeza ya mshahara haina mabadiliko hawakuona haja ya
kuendelea na majadiliano mpaka watakapowasiliana na wenzao. Waliahidi
kutoa taarifa ndani ya wiki mbili. Tarehe 12 Juni, 2012, Rais wa MAT
aliandika barua kwa Katibu Mkuu Utumishi ambaye ndiye kiongozi wa majadiliano
kwa upande wa Serikali, kuwa Madaktari wameikataa taarifa na ufafanuzi
waliopewa kutoka Serikalini kwa ujumla wake.

taaluma nyingine wenye shahada ya kwanza wanaoanza kazi ambao kwa wastani
hupata shilingi 446,100/=.

usumbufu wa kupata barua hizo na kuzijibu. Kwa nini upate usumbufu wa kuachishwa
kazi na kutakiwa kuondoka kwenye nyumba ya Serikali ndani ya saa 24.
Jiepushe na yote hayo kwa kujiondoa mwenyewe. Usipofanya hivyo, mwajiri
anakuwa hana jinsi bali kukuondoa kazini maana unakwenda kinyume na sheria za
kazi na maadili ya kazi ya udaktari.

wenzake katika ujenzi wa taifa. Kwa namna ya pekee namshukuru na kumpongeza
Bwana Juma Mgaza, kwa moyo wake wa huruma na upendo na kwa hatua alizochukua za
kumsaidia Dkt. Ulimboka.

Serikali kufanya hivyo. Dkt. Ulimboka alikuwa mmoja wa kiungo muhimu katika
mazungumzo baina ya Serikali na Madkatari. Ni kweli kwamba yeye si

No comments:
Post a Comment