Msemaji wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ )Col. Kapambala Mgawe |
Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema hayo jana wakati akihojiwa na kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One, kufuatia kuwepo kwa taarifa kuwa kuna mabomu yamerushwa upande wa Tanzania toka nchi jirani ya Malawi.
“Hali ya mpakani ni shwari na jeshi liko huko, kama hali ingekuwa mbaya tayari Mbeya ingekuwa imehamwa, wananchi wasiwe na wasiwasi kabisa hakuna mabomu yeyote yaliyorushwa,” alisema Mgawe.
Alisema taarifa zilizosambazwa kwamba kuna mabomu yamerushwa toka Malawi ni jambo ambalo limetengenezwa ili kuwatia hofu wananchi kwasababu tu kulikuwa na kutofautiana kati ya Tanzania na Malawi. Alisema suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na viongozi wa nchi hizo kwa njia ya mazungumzo.
“Sidhani kama Malawi wanaweza wakafikia hatua ya kurusha mabomu, taarifa hizi ni za uzushi, hata namba zilizoandikwa siyo za jeshi ni mtu ametunga tu,”alisema Mgawe.
Mgawe alisema hata hivyo JWTZ lipo katika harakati za kufanya utafiti kubaini mmiliki wa namba iliyotumika kusambaza ujumbe huo na kwamba pia inawezekana watu wakafanya hivyo kwa ajili ya kufanya biashara zao.
Kuhusu ushirikiano kati ya JWTZ na makampuni ya simu, alisema watawasiliana na wenye mitandao ya simu na kwamba hata hivyo wananchi wasiogope na kujenga hofu katika jambo ambalo siyo la ukweli na badala yake waendelee na shughuli zao kama kawaida.
1 comment:
curry 7
balenciaga shoes
bape clothing
russell westbrook shoes
calvin klein underwear
jordan shoes
paul george shoes
yeezy boost 350 v2
yeezy boost 350
curry 8
Post a Comment