Thursday, October 18, 2012

Serikali yachoka kuchokozwa :Yaanza kuwashughulikia Masheik wachochezi

Sheik Pondo Issa Ponda
Huenda sasa serikali ya Tanzania imeochoka kuchokozwa na baadhi ya viongozi wa dini na makundi ya watu wanatumia dini kuvuruga amani ya nchi.

Kufuatia kauli ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, zimeonekana wazi  kuichosha Serikali na kufikia mwisho wa uvumilivu.

Hapo jana Jeshi la Polisi lilitangaza kumtia mbaroni Sheikh huyo maarufu kwa kuhamasisha vurugu na maandamano ya mara kwa mara.
H
ata hivyo baada ya kukamatwa kwake Polisi ililazimika kutumia mabomu ya machozi, kutawanya waumini wa Kiislamu waliovamia Kituo cha Polisi cha Kati, ili kushinikiza Ponda aachiwe.

Tukio hilo, lilitokea jana saa 8 mchana, baada ya kundi kubwa kuvamia kituoni, ambapo polisi walilazimika kuwafukuza kwa kutumia mabomu ya machozi.

Kutokana na jeshi hilo, kujipanga vizuri huku likitumia magari yenye namba za usajili PT 2081, PT 1848, PT 2103, walifanikiwa kuzunguka mitaa yote ya katikati ya Jiji kuimarisha ulinzi.
Polisi wakidhibiti vurugu zilizotokea jana huko Zanzibar

 Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo na kusema wanaendeleza msako wa watu walioratibu maandamano hayo.

Alisema katika tukio hilo, watu kadhaa walitiwa mbaroni, akiwamo raia mmoja wa Rwanda aliyekutwa na panga, shoka ndogo na majambia.

“Tumefanikiwa kukamata watu kadhaa na tumewakuta na vitu mbalimbali vya hatari, vikiwamo mapanga, majambia na mashoka madogo madogo…hii inaonyesha wazi, walikuwa wamejiandaa kufanya fujo,” alisema Kova.

No comments: