Friday, October 12, 2012

Vurugu: Mtoto akojolea Quran Waislamu wafanya vurugu


Kundi la watu wanaosemekana kuwa ni Waislamu limevamia mahakama ya mwanzo ya Mbagala Kizuiani na kutaka kupiga mtoto mwenye umri wa miaka 12, kwa madai ya kukojolea msaafu. Inasemekana chanzo cha tukio hilo ni utani kati ya mtoto huyo na mwenzake ambaye ni muumini wa dini ya Kiislam.
Watoto wa shule wakifunika pua zao baada ya mabomu ya  machozi kulipuliwa na jeshi la Polisi kudhibiti vurugu za waislamu baada  ya mtoto mmoja mwenye miaka 12 kukojolea quran na waisalamu kuamua kufanya vurugu huku Mbagala nchini Tanzania.
 Mwenzake alikua ametokea madrasa na kutaniana kwao kukafikia kwenye dini, ambapo mtoto wa Kiislam akamwambia mshutumiwa kwamba akikojolea Quran atageuka nyoka au chura (vyanzo vingine vinasema alimwambia akikojolea msaafu, atakua chizi.) Mtoto huyo mshutumiwa akakojolea Quran hiyo kuonyesha hakuna kitakachomtokea katika ubishani wao huo.


Baada ya mwenzake kukokolea msaafu, mtoto wa Kiislamu alimtaarifu mzazi wake kuwa mwenzie kakojolea kuraani, na baadae wazazi wa watoto hao baada ya kufikishiwa tukio hilo la kukojolea kitabu hicho walikaa na kukubaliana kwenda mahakamani kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya makubaliano yao.
Kundi la waislamu wakidhibitiwa na Jeshi la Polisi

 Inasemekana hapo ndipo kundi la Waislamu likajitokeza na kutaka kujua kinachoendelea. Hapo ndipo vurugu zilipoanza na kusababisha uharibifu wa gari la mkuu wa kituo hicho ambalo limepasuliwa kioo cha nyuma pamoja na gari nyingine aina ya Noah pia limeharibiwa.


Vurugu ziliendelea baada ya kundi hilo kuvamia kanisa la Tanzania Assemblies of God Mbagala Kizuiani na kurusha mawe na kusababisha hasara mbalimbali.

Kamanda Kova amesema kuwa athari zilizotokea mpaka sasa ni kwamba tayari Watu hao wamevunja Makanisa Matatu na pia baadhi ya magari yalivunjwa vioo na barabara kufungwa, jambo lililolilazimisha Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya.

 Mkuu wa kikosi maalum kanda ya Dar es salaam, kamanda Kova alisema kuwa tukio hilo lisiwekewe uzito wowote, kwa sababu ni la kitoto na halikuwa na kusudi lolote.

Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewataka Waislamu kuwa na busara maana aliyefanya tukio hilo ni mmoja na sio kundi hivyo si sahihi kuvunja na kuharibu mali za kanisa kana kwamba kanisa ndio limemtuma.

litoa mfano ambapo Bwana Mtume S.A.W akiwa na watu wake msikitini alitokea mtu mmoja akakojoa eneo la msikitini. Waumini walitaka kumvamia kwa hasira lakini Mtume S.A.W aliwaambia wamwache amalize kukojoa kisha akawatuma wamwite na akaanza kumueleza sura ambazo zinafahamisha kuwa nyumba ya Mungu ni mahali patakatifu na hapafai kufanya kitendo kile.
Amewataka waislamu kuiga mfano wa Mtume S.A.W. na kuacha hasira; hasa ukizingatia aliyefanya kitendo hicho ni mtoto wa miaka 12.