Katibu Mkuu mpya wa CCM Abrahaman Kinana |
Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete amemteua Abrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kuchukua nafasi ya Katibu aliyemaliza muda wake Wilson Mukama.
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,ambacho kimepitisha uteuzi wa Katibu Mkuu mpya pamoja na timu nzima ya Sekretarieti ya chama hicho.
Kikao hicho kilijadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa na Mwenyekiti wa Chama Jakaya Mrisho Kikwete, ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na Mhe. Abdulrahaman Kinana .
Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
- Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
- Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Mhe. Vuai Ali Vuai.
- Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Mwigulu Nchemba.
- Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
- Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
- Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
- Katibu wa Itikadi na Uenezi- Nape Nnauye
Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.
2 comments:
pandora jewelry
supreme outlet
longchamp
moncler outlet
off white
longchamp
moncler jackets
yeezys
curry 6
pandora
find more information replica ysl find out here Ysl replica content replica bags china
Post a Comment