Rais Jakaya Kikwete |
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo,
Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kuomboleza vifo vya Wasanii watatu vilivyotokea
hivi karibuni katika mazingira tofauti.
Wasanii
hao ni Muigizaji wa Kundi la Kaole yaani Kaole
Sanaa Group, Marehemu Khalid Mohamed ‘Mlopelo’ aliyefariki dunia hivi
karibuni kutokana na maradhi yaliyokuwa yanamsumbua kwa muda mrefu.
Aidha
Msanii wa Filamu John Stephano Maganga alifariki dunia tarehe 24 Novemba, 2012
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Vilevile
usiku wa tarehe 27 Novemba, 2012, Msanii mwingine maarufu wa Maigizo ya
Vichekesho na Muimbaji wa Muziki wa Kizazi Kipya, Hussein Ramadhan Mkieti
maarufu kwa jina la ‘Sharo Milionea’ alifariki dunia kwa ajali ya gari
alilokuwa akiendesha, baada ya gari hilo kupinduka katika maeneo ya maguzoni
Songa, Wilayani Muheza katika Mkoa wa Tanga.
Marehemu Mkieti alikuwa njiani akielekea nyumbani kwao katika Kijiji cha
Lusanga Wilayani Muheza - Tanga.
“Nimeshtushwa
na kuhuzunishwa mno kutokana na taarifa za vifo vya Wasanii hawa ambao kwa
hakika mchango wao mkubwa katika Tasnia ya Muziki na Maigizo hapa nchini
ulikuwa unatambuliwa na kuthaminiwa na wananchi wengi. Pengo waliloliacha
Marehemu hawa ni kubwa na ambalo si rahisi kuzibika katika kipindi kifupi”,
amesema Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
“Kutokana
na msiba huu mkubwa, ninakutumia wewe Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo,
Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kwa kuwapoteza Wasanii hawa maarufu ambao
wameliletea heshima Taifa letu katika nyanja za muziki na sanaa kwa ujumla”, ameendelea
kusema Rais Kikwete na kuongeza,
“Kupitia
kwako, naomba unifikishie Salamu zangu za Rambirambi kwa Familia za Marehemu
Wasanii wote hao ambao najua machungu waliyo nayo kwa sasa ni makubwa, nami
naungana nao katika kuomboleza vifo vya wapendwa wao. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema
azipokee na kuzilaza mahali pema peponi Roho za Marehemu, Amina”.
Rais
Kikwete amewaomba Wanafamilia wote wa Marehemu wawe na moyo wa uvumilivu na
ujasiri katika kipindi chote cha maombolezo ya wapendwa wao kwani yote ni
mapenzi yake Mola. Aidha ameomba Rambirambi zake ziwafikie Wasanii wote nchini
ambao, katika kipindi kifupi kilichopita, wamewapoteza Wasanii watatu maarufu
ambao enzi za uhai wao wamesaidia sana
kuinua kiwango cha sanaa hapa nchini.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
27 Novemba, 2012
2 comments:
moncler jackets
jordans shoes
golden goose sneakers
yeezy 380
supreme
kyrie 5 shoes
nike react
golden goose
golden goose
golden goose sneakers
replica bags wholesale in divisoria more tips here g4o98e4h68 best replica ysl bags replica bags reddit next page m4k26y4h67 replica bags pakistan anchor w3f18w0p28 gucci replica replica bags turkey
Post a Comment