Rais Kikwete katikati akiwa na Rais Barak Obama pamoja na mkewe Michelle Obama |
Rais Obama akimkaribisha White House Rais Kikwete alipokwenda kumtembelea na kuvunja rekodi kuwa rais wa kwanza barani Afrika kukutana na Rais Barak Obama |
Rais Kikwete na Obama wakatika mazungumzo wakati walipomtembelea Obama nchini Marekani |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameeleza
furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumanne, Novemba 6, 2012 wa
Rais Barack Obama wa Marekani katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu katika
salamu za pongezi kwa kiongozi huyo wa Marekani ambaye amechaguliwa tena
na wananchi wa nchi hiyo kwa kipindi cha pili, Rais Kikwete amesema
“Nimepokea
kwa furaha na shangwe habari za kuchaguliwa tena kwako kuwa Rais wa Marekani
kwa kipindi cha pili. Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, na kwa hakika, kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kukutumia wewe na
kupitia kwako Chama cha Democratic pongezi nyingi kwa ushindi wako wa maana
sana.”
Ameongeza
Rais kikwete katika salamu zake hizo: “Kuchaguliwa kwako tena kuendelea kuongoza
nchi yako muhimu na wananchi wake, ni ishara ya wazi ya uaminifu na imani
ambayo wananchi wa Marekani wanayo katika uongozi wako wa mfano.”
Amesisitiza
Rais Kikwete: “Wakati unajiandaa kuchukua tena uongozi wa nchi hiyo katika kipindi
chako kipya, napenda kukuhakikishia msimamo wangu binafsi na ule wa Serikali
yangu kuwa tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa na wewe na Serikali yako
ya kutukuka, ili kuendeleza uhusiano bora ulioko kati ya nchi zetu mbili
ndugu.”
1 comment:
qzz0521
pandora charms
longchamp solde
jordan shoes
burberry outlet
true religion jeans
reebok trainers
coach outlet
michael kors outlet online
chrome hearts outlet
christian louboutin outlet
Post a Comment