Utafiti mpya unaonyesha asilimia 27 ya wanawawake wanafanya ngono kinyume na maumbile.
Mtafiti Mwanasayansi Irine Mremi, kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binaadamu nchini Tanzania (NIMR) ambaye aliwasilisha ripoti hiyo kwa niaba ya watafiti wenzake wa NIMR amesema katika utafiti walioufanya umebaini asilimia 26.5 ya wanawake hukubali kuingiliwa kinyume.
BAADHI ya wanawake kutoka katika Wilaya za Kinondoni, Tanga, Makete na Siha, wamekiri kufanya ngono kinyume na maumbile.
Mwanasayansi Irine Mremi kutoka (NIMR) alikuwa akiwasilisha utafiti uliofanywa na watafiti wa NIMR juu ya ufanyaji Ngono kinyume na maumbile katika kueneza maambukizi ya VVU/Ukimwi nchini na kuwasilishwa mbele ya Wanahabari na Watafiti jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mremi amesema wanawake hao wamesema chanzo kikubwa kinacho wapelekea kufanya ngono kinyume na maumbile ni kujipatia kipato zaidi, Kuogopa kupata Mimba, kulinda usichana wao na baadhi ya mila na tamaduni za baadhi ya makabila.
“ Utafiti wetu uliwahusisha wasichana na wanawake wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea na kada tofauti katika jamii kama wanafunzi, wafanyakazi, wahudumu bar, wauguzi, makahaba na akina mama wa nyumbani, katika maeneo hayo watu 903 walijitokeza wakiwepo pia wanaume ambao wal;ihusishwa katika utafiti huo,” alisema Mtafiri Irine.
Aidha alisema wakati wa utafiti huo wanawake 44 kati ya 166 waliohojiwa walisema kuwa wanafanya tendo la kujamiiana kinyume na maumbile ambayo ni sawa na 26.5% huku 76.4% ya waliohojiwa walidai kufanhamu njia hiyo ya kufanya mapenzi.
Wilayani Tanga ndio kumeonesha kukithiri kwa vitendo vya wanawake kufanya mapenzi kinyume na maumbe na wanaume kuwafanyia wanawake kinyume na maumbile ukilinganisha na Makete ambako bado kuna idadi ndogo.
Wanaume
waliohojiwa katika utafiti huo wamedai wao wanafanya kwa mtindo huo
kwaajili ya kupata raha tu na imani ya kuwa huko hakuna maambukizi ya
VVU/UKIMWI na wamekua wakitumia mafuta ya aina mbalimbali ilhali
matumizi ya mipira ikiwa ni hafifu kwani wakitumia mipira wamedai
kupunguza raha wanayo ipata.
Wanawake
pia wamedai baadhi ya tamaduni zao hasa maeneo ya Mwambao huko Tanga
msichana kuolewa na kukutwa usichana wake haupo (Bikira) ni aibu kwake
na wazazi hivyo hulazimika kufanya mapenzi kinyume na maumbile, huku
suala la Mimba nalo likichukua nafasi.
Watafiti
hao wamesema ufanyaji huo wa ngono kinyume na maumbile umekuwa
ukisababisha michubuko kirahisi na kuchangia maambukizi ya Ukimwi kwa
kasi tofauti na kutumia njia ya kawaida ya kujamiiana.
Aidha imedaiwa kuwa wanawake wengi wanaofanya ngono kinyume na maumbile wamekuwa wakipata shida wakati wa kujifungua kwa misuli yao ya kushindwa kuhimili kusukuma mtoto, jambo ambalo limekuwa likileta tabu kwa wahudumu wa Afya hasa wakunga ambao ni wachache mahospitalini kutumia muda mrefu kumhudumia mjazito mmoja huku wengine wakiendelea kuteseka wodini wakati wa kujifungua.
Watafiti
hao wameshauri elimu zaidi ya kujikinga na maambukizi ya ukimwi na njia
salama za kujamiiana kufundishwa mashuleni ili kuondoa dhana ya
kujamiiana kinyume na maumbile kuwa haiambukizi virusi vya Ukimwi.
Watafiti
walioshiriki katika utafiti huo ni pamoja na Akili kalinga, Elizabeth
H Shayo, Irene Mremi, Godlisten materu, Stella Kilima, Gibson
Kagaruki, Anjela Shija, Judith Msovela, Dk. Leornad Mboera, Dk.Julius Massaga, Kesheni Senkoro na Basiliana Emid wote kutoka NIMR.
2 comments:
yeezys
retro jordans
lebron 15 shoes
paul george shoes
golden goose sneakers
kyrie 4
kyrie 6
cheap jordans
yeezy boost
cheap jordans
you could check here replica ysl hop over to this website replica gucci handbags read more gucci replica bags
Post a Comment