Wednesday, January 16, 2013

Inauma sana!!!: Wanafunzi IFM waeleza wanavyolawitiwa

Wanafunzi wa IFM siku walipoandamana kwenda Wizara ya Mambo ya Ndani

SIKU moja baada ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), kuitisha maandamano kushinikiza ulinzi wa polisi kutokana na vitendo vya udhalilishaji, jana walielezea jinsi wanavyofanyiwa vitendo hivyo na wahuni.

Wanafunzi hao ambao wamepanga katika nyumba zilizoko Kigamboni, wamedai kudhalilishwa na wahuni hao kwa kuporwa vifaa vyao kama kompyuta, fedha na vitu vingine na hata kubakwa na kulawitiwa.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi IFM (IFMSO), Michael Charles jana alieleza jinsi udhalilishaji dhidi ya wanachuo wawili wanaume wa chuoni hapo ulivyotokea Januari 12, mwaka huu.
“Kulikuwa na wanafunzi wanne walikuwa wakijisomea chumbani kabla ya kuvamiwa usiku wa manane na watu wasiowatambua wapatao wanane.”



“Watu hao walikuwa wanataka kompyuta, simu, fedha na vitu vingine na vile ambavyo hawakuwa navyo, walizua tafrani kati yao... Hawa jamaa walikuwa kwenye nyumba yao iliyoko Uwanja wa Machava.”

“Katika sakata hilo, wanafunzi wawili walipata upenyo na kukimbia, lakini wawili walikosa na kuendelea kupambana na wahuni hao ambao waliwazidi nguvu kutokana na wingi wao na kuwaingilia kinyume na maumbile.”

“Kwa kweli ilituuma sana baada ya kupata bahari zile. Waliwadhalilisha sana... Jamaa walipora mali za wanafunzi hao na zaidi ni kompyuta, fedha na simu. Tumekuwa tukiripoti matukio haya mara kwa mara polisi, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwani vitendo hivi ni vya muda mrefu.”

“Kuna siku nyingine, wanafunzi walikuwa wakijisomea usiku, mara wakavamiwa na wahuni hao na walipotakiwa watoe kompyuta, simu na fedha na pale inapotokea hawakuwa navyo ama kuwabishia, basi wanajeruhiwa kwa mapanga.”

“Hiyo ni kweli kabisa, dada zetu wanabakwa sana tu ila hawasemi kwa kuogopa aibu katika jamii na hata taarifa zinapofikishwa polisi tunaishia kupewa RB tu halafu tunaambiwa watafuatilia.”

“Hawa watu si kwamba ni wageni, wanafahamika na hata maeneo yao wanayofanyia uharamia huo yanafahamika... Ukweli wanatunyima uhuru kabisa na tumesharipoti polisi lakini hakuna kinachoendelea. Tumeporwa zaidi ya kompyuta ndogo 300, kinachotuuma zaidi, hawa wezi wanafahamika wanapokaa na polisi inawaangalia.”

Wanafunzi wengine
Baadhi ya wanafunzi hao wanaoishi Kigamboni walidai kuwa wanaishi katika mazingira hatarishi kwani wakati mwingine uporaji hufanyika kweupe saa 11 jioni.

Maeneo yaliyotajwa kuwa ni hatari na wakazi wa Kigamboni ambayo wenyeji hulazimika kuyapita kabla ya saa 12:00 jioni ni Midizini, Minazi Mikinda, Mnara wa Rada, Kisimani na Serengeti.

Mwanachuo mwingine ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe alisema: “Tofauti za kimaisha baina yetu ndiyo zinazosababisha chuki kuwa wanachuo wanaringa na kujiona wenye hadhi za juu ndiyo maana wanafanyiwa vitendo hivyo.

Wakazi nao wanena
Baadhi ya wakazi wa Kigamboni walisema kuwa mji huo ambao umepangwa kuwa wa kitalii sasa si salama.

Mmoja wa wakazi hao ambaye pia aliomba jina lake lisiandikwe gazetini alisema inapofika saa moja usiku, vitendo hivyo vya uporaji wa kutumia mapanga huanza na kuongeza kwamba kinachowasikitisha ni Jeshi la Polisi kufumbia macho vitendo hivyo.

Mwingine alisema wamekuwa wakipata usingizi wa shaka kutokana na kujawa hofu kuwa muda wowote wanaweza kuvamiwa na kuporwa.

Wakazi hao walisema kutokana na wahusika kutochukuliwa hatua, wanashawishika kuamini kuwa kuna ushirika kati ya baadhi ya polisi na wahalifu hao.

“Wezi wote hapa tunawafahamu na polisi pia wanawafahamu, inasikitisha kwamba wanamkamata mhalifu, wanamfikisha kituoni na kesho anadunda mtaani kama kawaida,” alisema.

“Hali ya Kigamboni ni tete, mambo haya yalianza kidogokidogo lakini sasa yamekithiri na polisi wanajua... Nenda katika fukwe ambazo watu wanapumzika. Kuna uporaji na wakati mwingine hutokea mauaji,” aliongeza mkazi mwingine.

Wakati wakazi hao wakizungumza hayo, juzi Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwataka wanafunzi hao wanapoona kuwa matatizo yao hayashughulikiwi ngazi za chini, wayaripoti ngazi za juu.

Hata hivyo Kamanda huyo aliahidi kushughulikia matatizo hayo mara moja na kusema kwa kuanzia, ataongoza vijana wake kufanya msako wa wahalifu wote wanaohusika na vitendo hivyo.

Mbunge Kigamboni akiri
Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustin Ndungulile alisema eneo la Kigamboni kwa sasa si salama kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo vya uhalifu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Dk Ndungulile alisema uhalifu huo unachangiwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa ajira kwa vijana hasa baada ya kuzuiwa kwa shughuli za ujenzi kutokana na Mradi wa Ujenzi wa Mji Mpya wa Kigamboni.

“Taarifa ya vitendo vya uhalifu ninayo, baadhi ya wanafunzi walikuja kwangu kama mwezi mmoja uliopita na kunieleza matatizo yao na nikawasiliana na Mkuu wa Kituo cha Polisi Kigamboni, ambaye naye alinijulisha kwamba tayari wamewakamata vijana 15 wakihusishwa na vitendo hivyo.”

Mbunge huyo pia aliwataka wanafunzi pamoja na wananchi wengine wanaoishi jimboni mwake wenye taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa wahalifu zaidi wawasiliane naye mara moja.

Source:Mwananchi

4 comments:

yanmaneee said...

kd 10
yeezy boost
air jordan 1
supreme
jordans
air jordan
bape outlet
yeezy shoes
kevin durant shoes
supreme clothing

dyry said...

look at this website https://www.dolabuy.ru/ Click Here replica gucci bags get redirected here replica ysl

Anonymous said...

read this post here Dolabuy Loewe read dolabuy replica go to website Balenciaga Dolabuy

teatheth said...

dig this d6j71f0g72 bags replica gucci best replica ysl bags replica bags nyc hermes fake u4l82p3b91 7a replica bags wholesale replica goyard bags gucci replica handbags l9a63g4v41 replica bags gucci