Friday, April 26, 2013

Lema adai ametumiwa ujumbe wa vitisho na Mkuu wa Mkoa



Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amedai kupokea ujumbe wa vitisho kwa simu kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha, Lema alidai kuwa ujumbe huo umeandikwa kupitia simu ambayo namba 0752960276 na unaosomeka: “Umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”

Alisema baada ya kupata ujumbe huo, alimjibu kuwa “nimekupata nimekuelewa nipo tayari kwa lolote.”

Hata hivyo, Mulongo amekana kumtumia Lema ujumbe huo... “Nimepata hizi taarifa wewe ni kama mtu wa nane kuniuliza. Sijatuma huo ujumbe na siwezi kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”
kuwa na mawazo ya kumtumia ujumbe huo kwani kama ningetaka kumkamata tangu jana pale Chuo cha Uhasibu ningemkamata.”

Hata hivyo, alihoji sababu za mbunge huyo kujificha kama anajijua kwamba hana kosa. “Kwanza nani kamwambia anataka kukamatwa? Yeye anatakiwa kusaidia polisi, kwani wale vijana 13 waliokamatwa kwa ajili yake wapo mahabusu anasubiriwa atoe maelezo.”

Alisema Mbunge huyo, anajua kazi ambayo, ilifanya chuo cha uhasibu na ndiyo sababu anajificha... “Alifanya kazi yake nikazomewa, kama ningetaka kutumia madaraka yangu asingekuwa salama … nadhani Lema anahitaji kusaidiwa ili abadilike.”

Kuhusu madai ya kujificha, Lema alisema haitajisalimisha polisi licha ya Mulongo kuagiza akamatwe kwa kuwa kuna taratibu za kufuatwa polisi inapomhitaji mbunge ambaye amechaguliwa na watu.
Alisema kama polisi wanamuhitaji, wanapaswa kumuita na pia kuwasiliana na Ofisi ya Spika wa Bunge.

“Naomba ieleweke kuwa mimi sijawakimbia polisi, siogopi kesi na wala siogopi jela nitaendelea na shughuli zangu waje kunikamata barabarani,” alisema Lema.
Akizungumzia tukio la juzi, Lema alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa ndiye aliyekuwa chanzo cha vurugu kwa kukosa weledi wa kuzungumza na wanafunzi wenye majonzi.

Alisema alikwenda chuoni hapo baada ya kuitwa na wanafunzi na kabla ya kuzungumza, alikutana na uongozi wa chuo, akiwamo Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Arusha.

“OCD Arusha aulizwe kazi ambayo nilifanya kutuliza hasira za wanafunzi na tutasambaza DVD zaidi ya 3,000 kwa wakazi wa Arusha kujionea tukio hili ambalo sasa limebadilishwa na kuwa la kisiasa,” alisema Lema.

Mwanafunzi, Henry Kago(22) aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na watu wasiojulikana na kusababisha wanafunzi kucharuka chuoni hapo anatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Iringa kwa mazishi.

Source: Mwananchi

No comments: