Waziri wa Mambo ya nchi za nje na Ushirikano wa Kimataifa Benard Membe ameweka
hadharani yalipo moyoni mwake kuhusu mpango wake wa kugombea urais wa Tanzania.
Membe ambaye amekuwa akihusishwa na mpango huo amesema
atakuwa tayari kugombea nafasi hiyo mwaka 2015 kama wananchi wataona anafaa na
kumtaka afanye hivyo.
Membe aliyasema hayo mjini Iringa wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kongamano la kitaifa la Vyuo vikuu katika ukumbi wa St. Dominic.
Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo amesema
pamoja na kwamba wakati wenyewe haujawadia ambapo pia chama chake cha
mapinduzi hakijatoa utaratibu lakini atakuwa tayari kusikiliza ushauri wa
Watanzania.
“Naomba kurudia niliyowahi kusema kwamba muda haujafika wa kutangaza kugombea urais... lakini nasubiri sana ushauri wa watanzania. Iwapo wananchi watanishauri na kunitaka nigombee nitapima ushauri huo iwapo wananchi wengi watanitaka nifanye hivyo nitachukua fomu na kugombea kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu” Alisema Membe.
No comments:
Post a Comment