Sunday, June 9, 2013

Taifa Star yafungwa na Morocco 2 - 1 , Ivory Coast yaibanjua Gambia 3 - 0


Timu ya Taifa ya Tanzania inahitaji maajabu ili iweze kwenda Brazil kucheza kombe la dunia baada ya jana kufungwa na Morocco jumla ya magoli 2 - 1.

Tanzania ambayo ilionyesha udhaifu mkubwa katika kiungo na ushambuliaji ilistahili kichapo hicho kwani kwa wale wanaofahamu soka watukubaliana kuwa ilistahili kupata adhabu hiyo kwa vile Morocco walitawala mchezo huo kuanzia kipindi cha kwanza hadi cha pili.

Goli pekee la Taifa Stars lilifungwa na Amri Kiemba kwa shuti kali kutoka umbali wa mita kama 40.

Kwa matokeo hayo Tanzania inabakia nafasi ya pili na pointi 6 huku Ivory Coast wakiendelea kuongoza kundi C kwa kuwa na point 10 baada ya jana pia kuifunga Gambia jumla ya magoli 3 - 0.

Taifa Stars wanahitaji kushinda mechi baina yake na Ivory Coast siku ya  jumapili ijao katika uwanja wa Taifa ili kupunguza tofauti ya pointi. Mechi kati Ivory Coast na Stars itachezwa Jumapili hapa nyumbani kuanzia saa 9 alasiri.

 Msimamo kamili wa kundi C baada ya mechi za jana huu hapa chini

KUNDI C

TeamMP W D GF GA Pts
Ivory Coast431010210

Tanzania
4202666

Morocco
4121675

Gambia
4013291