Wednesday, November 17, 2010

Nahodha ateuliwa kuwa mbuge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewateua wabunge watatu akiwemo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha.
Wengine walioteuliwa ni pamoja Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Ndugu Zakia Hamdan Meghji.
Kwa mujibu wa Ibara ya 66 (1) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977, kama ilivyorekebishwa inampa mamlaka Rais ya kuteua Wabunge 10.
kwa mujibu wa Taarif kutoka Idara ya Mawasiliano ikulu Rais atateua wengine waliosalia siku zijazo.
Rais Kikwete ameshawasilisha majina ya wateule hao kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kwa ajili ya hatua ya kuapishwa

No comments: