Saturday, October 19, 2013

Mengi yaanza kuibuka sakata la Ufoo Saro

Ufoo Saro akiwa hosptali ya Muhimbili kwa matibabu

UTATA wa risasi umegubika tukio la kifo cha mzazi mwenzake na mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro, marehemu Anthery Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi. Utata huo umeibuka baada ya ndugu wa marehemu Mushi kushangazwa na kuhoji mazingira ya kifo cha ndugu yao anayedaiwa kujipiga risasi mbili kidevuni na kupoteza maisha papo hapo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni kaka wa marehemu, Isaya Mushi alisema familia imebaki kizani juu ya kifo cha ndugu yao na kwamba anayejua siri nzito juu ya kifo hicho ni mzazi mwenzake, Ufoo.


Tuesday, October 15, 2013

Kikwete uso kwa uso Ikulu na Lipumba, Mbowe na Mbatia

Rais Jakaya Kikwete
Freeman Mbowe
Prof. Ibrahim Lipumba
RAIS Jakaya Kikwete leo anakutana Ikulu na viongozi wa vyama vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi kwa ajili ya mazungumzo ya kuboresha kasoro zilizojitokeza kwenye muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013.

Hatua hiyo inatokana na msimamo wa wabunge wa vyama hivyo kususia mjadala wa muswada huo uliopitishwa hivi karibuni na wabunge wachache wa CCM na Augustine Mrema wa TLP, wakidai umechakachuliwa, huku Zanzibar ikiwa haijashirikishwa.

Monday, October 14, 2013

Ufoo Saro aondolewa risasi endelea vizuri MuhimbiliUfoo Saro katka hosptali ya Muhimbili
Ufoo Saro alivyowaokoa ndugu zake wasiuawe baada ya kupigwa risasi

Ufoo Saro baada ya kupigwa risasi

Mwandishi wa habari wa ITV, aliyejeruhiwa kwa risasi jana asubuhi, alilazimika kuvumilia majeraha ili kujiokoa yeye mwenyewe na wadogo zake watatu waliokuwa wakipigwa risasi, baada ya mama yake mzazi, Anastazia Saro (58), kuuawa.Mauaji hayo ya kusikitisha, yalifanyika katika eneo la Mbezi Kibwerere, nyumbani kwa mama yake Ufoo ambako alikuwa akiishi na wadogo zake Ufoo ambao ni Goodluck, Innocent na Jonas. 


Matuhumiwa wa unyama huo ametajwa kuwa ni Anthery Mushi, ambaye ni baba mtoto wa Ufoo, na siku ya tukio wawili hao walitokea Mbezi Magari Saba nyumbani kwa Ufoo, kwenda kuzungumza kifamilia na mama mzazi wa mwandishi huyo.

Ufoo Saro wa ITV apigwa risasi na mumewe aliyejiua na kuumua mama mkwe

Ufoo Saro akiwa hosptalini
MWANDISHI wa Habari ambaye pia ni Mtangazaji wa ITV, Ufoo Saro, amepigwa risasi na mchumba wake aitwaye Antel Mushi. Baada ya kufanya unyama huo, Mushi ambaye alikuwa Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini Sudan, alimuua kwa risasi mama yake Ufoo, Anastazia Saro (58) kisha naye akajiua.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri, eneo la Kibamba, Dar es Salaam. “Tukio hilo limetokea leo (jana), asubuhi saa 12 alfajiri eneo la Kibamba CCM, baada ya Mushi ambaye ni mzazi mwenzake na Ufoo, kurejea nchini juzi akitokea Sudan na kufikia nyumbani kwa Ufoo.

Sunday, October 13, 2013

Mwakyembe ajitosa kuokoa mabilioni kutokana na mgomo wa malori


Serikali imesema mgomo wa madereva wa malori umeyumbisha uchumi wa nchi na kuiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kufanyakazi saa 24, Bandarini Dar es Salaam ili kupunguza athari zilizilojitokeza.

Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), mapema wiki hii kilisimamisha kusafirisha mizigo na abiria nchi nzima kutokana na Wizara ya Ujenzi kuondoa nafuu ya kutolipa tozo ya uzito wa magari uliozidi asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria. 

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrisson Mwakyembe, alitoa agizo hilo wakati akipokea meli kubwa kutoka kampuni ya Maersk ya nchini Denmark yenye uwezo wa kubeba kontena 4,500 ambayo ni mara ya kwanza kuingia nchini kwa ajili ya majaribio.

Saturday, October 12, 2013

Zitto na tuhuma nzito kwa wabunge wa CCM kuhujumu Katiba


Zitto Kabwe

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema kuna njama inayofanywa na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutaka mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya usiishe ili wajiongezee muda hadi mwaka 2017.

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Kaskazini, alisema kuwa lengo la wabunge hao ni kutaka muda wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 usogezwe mbele hadi 2017 ili waendelee kukaa madarakani.
Alisema kuwa CHADEMA haitakubali uvunjwaji wa aina yoyote wa katiba, na hivyo kumtahadharisha Rais Jakaya 
Kikwete kutothubutu kukubaliana na fitna hizo.

Thursday, October 3, 2013

Mbeya kimenuka vurugu kubwa mgomo mashine za TRA chanzo

Askari wa FFU wakishika doria kuhakikisha 

 Polisi wa FFU wakidhibiti hali 
Baadhi ya vijana walichoma matairi
WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamezua kizaazaa wakigoma kufungua maduka wakipinga agizo la Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) linalowataka kununua mashine za kielektroniki kwa ajili ya kukatia risiti za wateja pindi wanapowauzia bidhaa.

Katika sokomoko hilo lililotokea jana na kusababisha taharuki kwa muda kadhaa, wafanyabiashara hao wanadai kuwa gharama za mashine zitolewe na serikali.
Eneo la Soko la Sido ambalo lina wafanyabiashara wengi na tegemeo katika uchumi wa Jiji la Mbeya, walifunga biashara zao kwa muda usiojulikana.

Wednesday, October 2, 2013

Mapya yaibuka kwa Mkenya aliyeachiwa kesi ya kumteka Dr Ulimboka

Mkenya Joshua Mulundi aliyeachiwa baada ya kulipa faini ya Sh. 1000/=


Mkenya Joshua Mulundi aliyeachiwa huru baada ya kulipa faini ya Sh1,000 kwa kupatikana na hatia ya kuidanganya polisi kuwa alihusika kumteka na kumjeruhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka amesema alitishiwa bunduki na kutekwa kabla ya kufikishwa mahakamani.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimhukumu kifungo cha miezi sita jela au kulipa faini hiyo. Mulundi alilipiwa faini hiyo na Mwandishi wa Habari wa Redio Times, Chipangula Nandule.