Sunday, February 13, 2011

Mubarak ang'oka Misri Jeshi lashika hatamu


Jeshi la Misri limesisitiza kuwa litazingatia makubaliano yote ya kimataifa.

Tangazo hilo ambalo limesomwa na afisa wa ngazi ya juu wa kijeshi kupitia televisheni ya taifa, amethibitisha kuwa makubaliano ya amani ya Misri na Israel yatabakia vilevile.

Jeshi pia limeahidi kusimamia mabadiliko ya amani kwenda kwenye utawala wa kiraia.

Taarifa hiyo imekuja wakati maelfu ya waandamanaji wakisalia katika eneo la wazi la Tahrir mjini cairo, wakisherekea kujiuzulu kwa rais Hosni Mubarak siku ya Ijumaa.

"Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ina nia ya kutekeleza makubaliano na majukumu yote ya eneo letu na kimataifa," amesema afisa huyo wa jeshi.


Kuondoka kwa Bw Mubarak kumepokewa kwa hali ya mashaka na wanasiasa wa Israel, wakiwa na wasiwasi huenda mabadiliko ya utawala yakahatarisha makubaliano ya amani ya mwaka 1979 yaliyofikiwa Cam David.

Jeshi pialimesema limeitaka serikali iliyopo kuendelea kusalia madarakani, hadi serikali mpya iyakapoundwa, ambayo itafungua njia kwa utawala utakaopatikana kwa njia ya uchaguzi.

No comments: