Sunday, April 10, 2011

Kikwete na Siri kubwa Moyoni


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kutangaza Sekretarieti mpya ya chama hicho baada ya iliyokuwa inaongozwa na Katibu Yusuf Makamba kujiuzulu hapo jana.

Hadi sasa bado haijafahamika ni nani atachukuwa nafasi ya Makamba japo kuna kila dalili kuwa Katibu Mkuu mpya wa chama hicho huenda akawa na haiba ya ujana kufuatia maneno yaliyowahi kusemwa na Mwenyekiti wa Chama hicho kuwa chama hicho kinahitaji kujivua gamba na kuwapa nafasi vijana ili kukiimarisha.

Wengi wamekuwa na hisia tofauti kuwa ni nani ataukwaa ukatibu mkuu wa chama hicho ambapo tayari makada kadhaa vijana wameanza kutabiriwa huenda wakachukua nafasi hiyo.

Miongoni mwa wanaotajwatajwa ni Kada maarufu wa Chama hicho Nape Nnauye, Amos Mkala na Benard Membe. Hata hivyo siri ya nani ataikwaa nafasi bado ipo moyoni mwa mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete.

No comments: