Thursday, June 30, 2011

Entencelles kwaheri ,Simba yaunguruma CECAFA


Timu ya Etincelles ya Rwanda imekuwa ya kwanza kuyaaga mashindano ya CECAFA Klabu Bigwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kufungwa kwa mara ya tatu mfululizo pale ilipofungwa na Red Sea ya Eritrea jumla ya magoli 4 – 1 katika mchezo wa awali ulifanyika katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Tanzania.

Katika mechi ya awali Etincelles ilifungwa na Zanzibar Ocean View 3-2 na baadae ikafungwa na Vital’o ya Burundi magoli 3-1.

Katika mechi ya pili iliyochezwa katika uwanja huo huo wa Taifa mjini Dar es Salaam Simba ya Tanzania imepata ushindi wake wa kwanza baada ya kuifunga timu ya Ocean View ya Zanzibar goli 1-0

Bofya hapa kwa picha na habari zaidi

No comments: