Sunday, October 21, 2012

Polisi: Hatuhusiki na kupotea kwa Sheikh Farid

Kamshna wa Polisi Zanzibar Musa Ali Musa
Jeshi la Polisi Viwani Zanzibar limekanusha vikali kuhusika na kupotea kwa Sheik Farid Hadi Ahmed Kiongozi wa kundi la Uamsho ambaye alipatikana juzi usiku baada ya kupotea kwa siku tatu na badala yake limesema linamhoji Sheikh huyo aeleze alikuwa wapi kwa muda wote huo .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamishna wa Polisi viwani Zanzabar Musa Ali Musa amesema Jeshi lake halihusiku kwa namna yoyote kama ambavyo Sheikh huyo alinavyodai.

Baada ya kurudi alikokuwa ametoweka Sheikh Farid anadai alitekwa na watu wenye bunduki waliokuwa wamefunika nyuzo zao ambao pia walimfunika macho kwa kitambaa na kumpeleka mahali pasipo julikana ambapo walimhoji mambo mbali mbali.

Sheikh Farid Hadi Ahmed (Picha kwa hisani ya Global Publishers)
Kamishna Musa anasema kwa sasa Jeshi la Polisi linamhoji ili aeleze alipokuwa kwa muda wote ili kujua ukweli wa sakata hilo

"Jeshi la Polisi linakanusha katika sakata la kutekwa kwa kiongozi huyo wa Uamsho ... tunamhoji kujua ukweli wa tukio hilo zima". Amesema

Hadi sasa haijajulikana Jeshi la Polisi litachukua hatua gani dhidi yake baada ya kumhoji baada ya matukio kadhaa yaliyoambatana na kutoweka kwake kutikisa visiwa vya Zanzibar

Katika siku tatu mfuliluzo baada ya kutoweka kwake wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa kundi la Uamsho walifanya vurugu ikiwa ni pamoja na kuchoma makanisa na kuharibu mali.


2 comments:

oakleyses said...

ferragamo shoes, soccer shoes, nike roshe, nfl jerseys, vans outlet, jimmy choo shoes, beats headphones, reebok shoes, valentino shoes, lululemon outlet, birkin bag, p90x workout, ugg outlet, asics shoes, mac cosmetics, longchamp, hollister, mcm handbags, ugg, babyliss, marc jacobs outlet, north face jackets, insanity workout, celine handbags, soccer jerseys, uggs on sale, canada goose outlet, wedding dresses, uggs outlet, replica watches, uggs outlet, canada goose, nike huarache, north face jackets, ugg boots clearance, mont blanc pens, instyler ionic styler, herve leger, nike trainers, canada goose outlet, canada goose outlet, giuseppe zanotti, new balance outlet, bottega veneta, ghd, ugg boots, chi flat iron, abercrombie and fitch, ugg soldes

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans