Sunday, October 28, 2012

Sakata la Vigogo kuficha fedha Uswis: Zitto kuwasilisha hoja binafsi

Zitto Kabwe
 Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe, anatarajia kuwasilisha hoja binafsi katika mkutano wa tisa wa Bunge unaotarajiwa kuanza wiki ijayo mjini Dodoma, kutaka serikali irejeshe fedha za vigogo wanaodaiwa kuzificha Uswis linaripoti gazeti la Mwananchi.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, amesema tayari hoja hiyo imeshapata baraka za Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Mbunge huyo wa CHADEMA alisema hayo jana wakati wa akifunga mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Nanjarareha, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.Katika uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika leo, CHADEMA imemsimamisha, Frank Salakana. Alisema sh bilioni 349 zilizofichwa Uswisi na baadhi ya vigogo wa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM), lazima zirejeshwe nchini, huku akimtaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Edward Hosea, kueleza umma barua aliyoituma nchini humo kwa ajili ya kashfa hiyo ilikuwa na lengo gani.

Alisema barua ya Dk. Hosea imesababisha ugumu wa upatikanaji wa taarifa za mabenki ya nchini Uswisi ambayo yameshindwa kutoa ushirikiano kwa kamati inayofuatilia kashfa hiyo.
Huku akishangiliwa na maelfu ya wanachama wa CHADEMA waliofurika kusikiliza mkutano huo, Zitto alisema wizi wa mabilioni hayo umetokana na kuporomoka kwa maadili ya viongozi nchini ambao wengi wanajali zaidi masilahi binafsi badala ya umma.
Mbunge huyo machachari wa CHADEMA, alisema kuna haja kama taifa kurejesha maadili ya uongozi kama enzi za utawala wa Mwalimu Nyerere ili viongozi wachague kitu kimoja, kati ya biashara na siasa.
Alisema CHADEMA imepania kuhakikisha mabilioni hayo yanarejeshwa ili yaweze kutumika kuwasaidia Watanzania katika kujenga na kuboresha miundombinu ya barabara, maji na afya.
Aliwataka viongozi walioficha mabilioni hayo kujitokeza mapema na kueleza jinsi walivyozipata badala ya kusubiri kuumbuliwa.
“Nawataka viongozi waliohusika wajitokeze wenyewe, waeleze walivyozipata na kisha wazirejeshe nchini, vinginevyo patachimbika, kwani nitahakikisha kama chama tunashirikiana na Benki ya Dunia kuhakikisha fedha hizo zinarudi nchini,” alisema Zitto.
Alisema CHADEMA inapigania fedha hizo zirejeshwe kwani zimetokana na wizi wa rasilimali za Watanzania kupitia mikataba mibovu ya mafuta na wizi wa madini na nyingine.
Katika ripoti ya Swiss Central Bank, iliyotolewa hivi karibuni, inaonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 11 barani Afrika ambazo vigogo wake wa kibiashara, kitawala na kisiasa wameficha kwa siri mabilioni ya fedha katika mabenki ya Uswisi.
Nchini nyingine za Afrika zilizoficha fedha hizo ni Kenya, Uganda, Zimbabwe, Misri, Shelisheli, Afrika Kusini, Rwanda, Sierra Leone, Somalia na Sudan.
Kwa upande wa Tanzania, mapesa ambayo yamefichwa huko ni dola milioni 196.87, sawa na shilingi za Tanzania bilioni 315.5!
Hebu jiulize; mapesa haya tuliyoibiwa yangetusaidia kiasi gani kama yangerejeshwa nchini na kutumbukizwa kwenye miradi ya kuboresha huduma za jamii?
Pia jiulize swali jingine: Je, hata baada ya Benki Kuu ya Uswisi kuturahisishia mambo kwa kututobolea ukweli kwamba tumeibiwa, na kwamba wezi wetu wameficha hizo fedha nchini mwao, watawala wetu wana dhamira ya kuanzisha mchakato ili wahusika wafikishwe mahakamani na fedha hizo zirejeshwe nchini?

4 comments:

oakleyses said...

chanel handbags, burberry outlet online, christian louboutin outlet, nike air max, oakley vault, tiffany and co jewelry, michael kors outlet online, michael kors handbags, burberry outlet online, ray ban sunglasses, michael kors outlet store, prada handbags, oakley sunglasses, kate spade outlet, christian louboutin shoes, michael kors outlet, longchamp handbags, christian louboutin, coach outlet store online, true religion outlet, louis vuitton outlet, longchamp outlet online, nike free, true religion, polo ralph lauren outlet, gucci handbags, louis vuitton handbags, coach outlet, louis vuitton outlet, prada outlet, nike air max, jordan shoes, nike outlet, polo ralph lauren, louis vuitton, longchamp outlet, red bottom shoes, tory burch outlet online, kate spade outlet online, michael kors outlet online, coach purses, ray ban outlet, michael kors outlet online, coach outlet, tiffany jewelry, cheap oakley sunglasses, louis vuitton outlet online

oakleyses said...

true religion jeans, sac louis vuitton, sac michael kors, vans pas cher, lacoste pas cher, timberland, chaussure louboutin, nike roshe, tn pas cher, true religion outlet, louis vuitton pas cher, nike air max, nike blazer pas cher, michael kors canada, nike air max, new balance pas cher, nike free, air max, sac vanessa bruno, hollister, mulberry uk, longchamp pas cher, ray ban pas cher, burberry pas cher, lululemon, nike air force, ray ban uk, ralph lauren, oakley pas cher, hermes pas cher, louis vuitton, air jordan, michael kors uk, nike roshe run, air max pas cher, north face, scarpe hogan, louis vuitton uk, nike free pas cher, longchamp, north face pas cher, hollister, ralph lauren pas cher, converse pas cher, barbour, guess pas cher, abercrombie and fitch

oakleyses said...

ferragamo shoes, soccer shoes, nike roshe, nfl jerseys, vans outlet, jimmy choo shoes, beats headphones, reebok shoes, valentino shoes, lululemon outlet, birkin bag, p90x workout, ugg outlet, asics shoes, mac cosmetics, longchamp, hollister, mcm handbags, ugg, babyliss, marc jacobs outlet, north face jackets, insanity workout, celine handbags, soccer jerseys, uggs on sale, canada goose outlet, wedding dresses, uggs outlet, replica watches, uggs outlet, canada goose, nike huarache, north face jackets, ugg boots clearance, mont blanc pens, instyler ionic styler, herve leger, nike trainers, canada goose outlet, canada goose outlet, giuseppe zanotti, new balance outlet, bottega veneta, ghd, ugg boots, chi flat iron, abercrombie and fitch, ugg soldes

oakleyses said...

pandora jewelry, swarovski jewelry, ray ban, timberland shoes, canada goose, pandora uk, hollister, ugg, uggs canada, nike air max, karen millen, toms outlet, moncler outlet, coach outlet, lancel, moncler, hollister clothing, juicy couture outlet, baseball bats, juicy couture outlet, pandora charms, moncler, louboutin, links of london uk, supra shoes, parajumpers outlet, wedding dress, air max, canada goose, replica watches, moncler outlet, converse shoes, canada goose pas cher, moncler, gucci, ralph lauren, moncler, montre femme, swarovski uk, oakley, louis vuitton canada, moncler, converse, thomas sabo uk, canada goose, hollister canada, iphone 6 case, vans