Wednesday, December 12, 2012

Papa hatimaye aingia ndani Tweeter, atweet maelfu wamfuatilia kwa dakika

Papa Benedicto XVI


Kwa mara ya kwanza Papa Benedicto XVI leo ameanza kutweet katika mtandao wa Tweeter.
Kama ambavyo ahadi kutoka Vatican ilikuwa wiki kadhaa huko nyuma, hatimaye baada ya kusubiri kuanzia usiku wa saa sita, kiu ya wafuatiliaji wa Papa kwa njia ya mtandao wa kijamii ya twitter imeanza kukatwa, mara baada ya Papa ku-tweet kwenye ukurasa wake.

Taswira ya takwimu mnamo dakika ya 52 baada ya kutweet.Dakika 45 baada ya tweet yake kuwa hewani, tayari wafuatiliajji zaidi ya 15,000 wali-itweet kwao.
Kadri dakika zilivyokuwa zinasogea, ndivyo tweet yake ilikuwa 're-tweeted' na maelfu zaidi ya watu. Tazama picha ambazo GK imenakili kutoka ukurasa wake, na namna zilivyokuwa zikibadilika kwa muda mchache.

Taswira ya tawkimu ilipofika dakika ya 55.Ilipofika lisaa limoja, tayari re-tweets zikawa 19,285, na ikawa favorite tweet kwa watu 5,954
Tweet ya Pili
Takriban baada ya dakika 45 za kutweet kwa mara ya kwanza, hatimaye Papa Benedict alikuja na tweet ya pili, na hapa hili lilikuwa ni swali kwa kila mtu, akiuliza ni namna gani tunaweza kusheherekea mwaka wa imani vema katika maisha yetu.

Tweet ya pili, ikiwa ni swali toka kwake.
Hapa napo kulikuwa na followers takriban elfu moja na kitu, ingawa hawakufikia wale wa tweet ya kwanza. Watu kadhaa walijaribu kwa kueleza ni namna gani tunaweza kufikia hiyo njia, kama ambavyo Papa aliuliza. Dakika tatu baadae, jibu likaja kutoka kwa kiongozi huyo mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni.
Tweet ya Tatu
Hili ndilo jibu ambalo Papa alikuja kuwawekea wananchi, baada ya kuwafanya watafakari kwa dakika tatu, wengine wakikaribia jib u, huku wengine wakishindwa hata kufikiri, na kuishia kkusema Ahsante kwa tweets zake. Na wapo poa waliodhani kuwa Papa anauliza ili apate ufahamu wao, lakini baadae wakaja kushtuka kuwa lilikuwa ni swali kama anavyouliza mwalimu darasani, na kisha kutoa jibu baadae.
Tweet ya tatu ikawa ni jibu la tweet ya pili, ambalo ni swali.

Hii ni historia ya aina yake kwa Baba mtakatifu Benedict wa 16, kutumia vema mitandao ya kijamii, ambapo lugha iliyotumika kwa tweet hizi za awali imekuwa lugha ya Kiingereza, japokuwa atakuwa anatumia lugha rasmi 7, ambazo ni Kiarabu, Kiingereza, Kiitaliano, Kireno, Kifaransa na Kijerumani na Kihispania.

Tweet ya kwanza, lakini katika ukurasa wake wa lugha ya Kifaransa.
Miongoni mwa lugha zote anazotumia, lugha yenye wafuatiliaji wengi imekuwa kiingereza, zingine zikiachwa kwa mbali.

Tweet yake ya kwanza, lakini katika lugha ya Kiarabu.
Unaweza kufuatilia tweets za Papa kupitia ukurasa wake wa @Pontifex. Picha zote zimenakiliwa kutoka ukuraasa wake na mwandihsi wa Gospel Kitaa.

No comments: