Thursday, January 17, 2013

Mkapa na Msuya Watoa Maoni ya Katiba Mpya



Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa (kulia) akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani (katikati) na Dkt. Salim Ahmed Salim. Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu  (Jumatano, Jan 16, 2013) jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya.

Mkapa akiendelea kutoa maoni

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akibadilishana mawazo na Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam  (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya

Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa akifurahia jambo na Wajumbe wa Tume na Sekretarieti ya Tume Mabadiliko ya Katiba jijini Dar es Salaam (Jumatano, Jan 16, 2013). Wajumbe wa Tume walikutana na Rais huyo Mstaafu leo jijini Dar es Salaam ili kupata maoni na uzoefu wake katika uandishi wa Katiba Mpya. Kushoto ni Mwenyekiti Jaji Joseph Warioba na kulia ni Mjumbe wa Tume Dkt. Salim Ahmed Salim, Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Cleopa Msuya akiongea na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu mchakato wa Katiba Mpya (Jumatano, Januari 16, 2013) jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba.
Picha na Tume ya Katiba.