Saturday, August 31, 2013

Salamu za baadhi ya viongozi ibada kuaga mwili wa Askofu Kulola

Add caption





Zifuatazo ni nukuu za baadhi ya viongozi mbalimbali ambao wako kwenye msiba wa Askofu Mkuu Dkt Moses Kulola ambaye amepumzika siku ya Alhamisi.  sehemu ya kwanza ya nukuu hizi kutoka kwa viongozi hawa, fuatana nasi.


Mh. Mbunge, Dr Getrude Rwakatare.
1976, alipohubiri nilikuwa na matatizo ya ndoa, nilipookoka bado nilikuwa na mateso ya ndoa, nikamuuliza mbona hivi? Akachukua jukumu la kuniandikia barua moja kila mwezi, na kuniambia hakupigi wewe anampiga Yesu, hakutesi wewe, anamtesa Yesu. Alinitia moyo hadi nilipokuwa mchungaji.

Alipokuwa anapelekwa India kwa ajili ya matatizo, nilipata nafasi ya kwenda kumuona Chanika, akaniombea na kunitamkia maneno kwa dakika 15, nikaona kama nimependelewa, na maneno ya mwisho na usia ili niweza kuendelea kumtendea kazi Mungu.

Baba amefanya kazi nzuri sasa ni sisi kuweza kufanya kazi ya BWANA bila kujihurumia.

Bishop Dr Methud Lyamungu, Methodist Church
NImekuwa nikimfahamu Kulola, juzi tu nilipofika uwanja wa ndege nikapokea msg kuwa hatunaye, amepumzishwa, ilikuwa shock, lakini namshukuru Mungu.
Nakumbuka miaka ya late 80's kulikuwa na mkutano kwenye kanisa la udugu, nikamwalika kwa chakula cha jioni, alikuja, nikashangazwa na unyenyekevu wake, ni rafiki wa wote, hana adui.

Askofu Esambu Mitachi Polo;
Bila Kulola sijui ningekuwa wapi, huduma yangu imeinuliwa na makanisa ya Ask. Moses Kulola. Lakini mkumbukkue hivi ndugu zangu, msafara wa mamba, kenge wapo. Yesu ndie muweza yote na yeye ndiye aliyezungumza haya.

Tunaweza kuzungumza maneno mazuri, lakini matendo hatuna. Tumtazame Yesu, maana hata huyu aliyetuacha, alikuwa anatuasa tumtazame Yesu, huwezi kuingia mbinguni bila mamlaka ya Bwana Yesu, usiwe kenge.

Tanzania tumtazame Yesu. Moses amekwenda, lakini Yesu yupo, amefanya kazi zake atalipwa na Bwana Yesu, na wewe ufanye kazi zako utalipwa na Bwana Yesu. Kiburi kitu kibaya, unafiki kitu kibaya, haya ndio maneno nayosema kwa Watz.

Phillip Mangula (makamu m/kiti wa CCM bara)
Moses nimeanza kumfahamu 8 /8/1083 nikiwa mkuu wa wilaya ya Kwimba, kipindi kile mtakumbuka kulikuwa n tofauti kidogo ndani ya kanisa, barua iliandikwa nchi nzima ya kuzuia Moses Kulola asihubiri kwa jina la kanisa, na mi niliipata kwangu.
Nikamweleza Moses Kulola, akaniambia, kijana wangu, mimi sitahubiri kwa jina la kanisa lolote, nitahubiri kwa jina la Yesu.

Nikawaita OCD, kwamba bwana, Moses Kulola hatahubiri kwa dhehebu lolote, atahubiri kwa jina la Yesu.

Tareje 9, tumemaliza mkutano, alihubiri mkutano mkubwa sana, mke wangu akajifungua mtoto wa kiume, nikamwita Moses, kwahiyo mtoto wangu anaitwa Moses Malumbo Kulola.
Dakika 20 baada ya kifo cha Dr Moses Kulola, nilipata msg, wakati huo nilikuwa nimetoka Njombe kumzika binti yangu wa mwisho, kipindi ambacho Moses, mtoto wangu alikuwa anaoa, Moses anao, dada yake mdogo anafariki, kwahiyo nilichelewa kidogo, lakini nimefika kushuhudia.

Alipotoka India alikuja na mwanae huyu hapa, tulizungumza mengi sana, lakini haoa si mahala pake, itoshe tu kusema, Moses alikuwa mtu wa watu. Aliendeleza injili, nasi tuiendeleze.

Theresia Uvinza
Nimemfahamu 1985, baada ya kumaliza chuo kikuu nilienda kufundisha Songea Girls, na hapo kulikuwa na rafiki yangu, Mama Hyela, walokole wa kwanza Songea. Siku moja aliomba nimshikie wanafunzi kwa kuwa mchungaji alikuwa anafikia kwake.

Nikamuuliza huyu mchungaji anafanana na Yesu?Akasema pengine, ila ukitaka kumuona, unaweza maana amefikia kwangu. Tukawaacha wanafunzi wote, tulifanya hilo kosa…

Tukasubiri na kusubiri na mida ya saa tisa, alipotoka nikajisikia kupiga magoti, nikamwambia baba naomba uniombee – na kweli akaniombea, nilikuwa na shilingi elfu moja tu, nikampa. Naamini mafanikio niliyo nayo ni kutokana na maombi niliyofanyiwa mwaka 1985.

Kwa hiyo kila wakati ambapo nilikuwa nikisikia Moses Kulola amekuja DSM, kwenye viwanja vya Jangwani , huwa sikusita kuhudhuria, labda tu niwe nje ya Dar. Nakumbuka aliwahi kusema nywele zake zilikuwa zinampotezea muda, hivyo akamuomba Mungu zibaki hivyo hivyo, na kweli zikabaki. Huu ni ushahidi kwamba kuna alikuwa anazungumza na Mungu.

Advera Senso (Msemaji wa Jeshi la Polisi)
Hata kama leo tungeamua takamate watenda dhambi wote, si kwamba wangebadilisha matendo yao kiroho na kimwili.

Amekuwa pia akimbwambia IGP Said Mwema, kuwa unpoona makosa ya jinai yanaongezeka hizo sisi watumishi wa Mungu tunaita dhambi, amwambie ili atume watu ama aende mwenyewe kuhubiri.


Hivyo tumekuwa tukiona makosa yakizidi sehemu, tunawasiliana na yeye anaenda kuhubiri injili eneo hilo.

IGP anasema chipukizi waendelee kuhubiri injili, hadi kweny ngazi ya familia, kwasababu wahalifu wako kwenye familia, wako kwenye mitaa…



Na watu wa Mungu niwawambie kuwa tushirikiane na serikali kuhakikisha kuwa wahuni wachache hawabadilishi amani iliyopo. Tuendelee kuhubiri na watu waokoke.

Paulo
Nashangaa kwa nini nimekuuja hapa, nitazungumza kidogo tofauti na m/kiti wangu.
Nilianza kumfahamu kaka yangu mwaka 67, akiwa ndio ameanza kazi kipindi hicho, nikawa namshangaa sana, nasema huyu mbona anapoteza muda, anazunguka na baiskeli huku na huko nikasema hapa tuna kazi kilichonipa faraja ni pale nilipoanza kuanza kazi yake.

Faraja niyoipata ni pale alipokuja Kilimanjaro, kipindi ambacho alinyimwa kuhubiri. Akaja kunionmba msaada ofisini, nikamwambia nani amekwambia akasema, aah aah, ni hilo ni nimekufikishia.

Nikamwambia kwa jina la Yesu utahubiri. Tukasimamia akafnya mkutano mkubwa sana, na lipomalia akaja ofisini kwanguna kuniambia sina cha kukulipa, piga magoti.

Akaniambia nitakuwakiongozi mzuri, baada ya hapo haikuchukua muda nikapelkwa Mbeya kama mkuu wa mkoa. Baraka zikaendelea, nikapata na uwairi, na tena uwaziri mwingine… nikakoswakoswa kidogo niwe waziri mkuu.

Assumpta Mshama (Mh Mbunge Nkenge/Mchungaji Msaidizi, Mito ya Baraka)
Watz, hatuna haja ya kuendelea kulia, sanasana ni kumshukuru Mungu… Hata ubunge huu nilipoupata, ni kipande kidogo cha Mzee huyu…

Wakati naokoka, 1989 kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, nilipoongozwa na mtu ambaye hata pia hajaokoa.

Nilipookoka kazi yangu ilikuwa ni kupika chakula na kumpelekea mahali popote. Na pia baadae nikaanza kurekodi video za mikutano yake.

Nilipotaka kuwa Mbunge, akaniambia utakuwa mbunge – na nilifanikiwa.

Mary Alice Chipungahelo (former RC, DSM)
Nilipoteuliwa kuwa RC, wakaniambia utaweza, nikasema zaidi ya hilo, nitapambana usiku na mchana…

Baba, sasa ni hayati Moses Kulola, alikuwa karibu na mimi sana, na kila anapokuja DSM, lazima anitembelee, Baba huyu, nilikuwa na matatizo, “mwanamke naye nini, mwanamke naye nini”
.
Alikuja nyumbani, nikamkaribisha nikapiga magoti, akauliza una nini, nikamwambia nataka natakasika. Mungu alizidi kuniunganisha naye, nikiwa Mwanza, aliwekwa ndani, nilipopata taarifa, tukapelekeana simu – lakini kama unavyojua kila mka na taratibu zake. Tulikubaliana mzee akatolewa, na akaja kunitafuta ili anie shukurani, nikamwambia hapana shukurani mpe Mungu, maana ndio ametuwezesha.

“Piga magoti” akaniambia, “unataka nini”, nikamwambia nataka niwe na afya nifanye kazi bila upendeleo wala rushwa.

Na ikawa hiyvo, nikapaishwa hadi Canada nikawa msaidizi wa Balozi, kazi ya heshima sana. Nimekuja kw moyo mweupe kabisa moyo mkunjufu, mama nikwambie kuwa wajane tuko wengi, wewe umebahatika kuwa na mzee anayeikjua dini, sisi wengine tumeolewa olewa tu…

Tunakutakia kila kheri, afya njema, ulee watoto, na watoto nao wana watoto wao

Kwa hisani : Gospel Kitaa

Nukuu zaidi za viongozi mbalimbali ni kwa hisa

No comments: