Saturday, September 14, 2013

Mwana FA achafuliwa jina baada kutoa ahadi msibani

Mwana FA , Mwanamuziki wa kizazi kipya

Mama wa Mwana Hip Pop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa mitindo huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia Costantine Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya Hamis Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia mitini.
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo (MwanaFA) ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha msanii mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani hitimisho la ahadi aliyoitoa kwa familia ya marehemu.
Tarehe 31 ya mwaka huu ilikuwa ni tarehe ya onesho la The Finest ambalo MwanaFA alikuwa akitimiza miaka 13 ya muziki wake, akawa na lengo pia na kuugeuza muziki wa Hip Hop uwe na sura ya kistaarabu na kibiashara pia ili kuuongezea aina ya mashabiki.
Siku moja kabla ya onesho, msiba wa Albert Mangwea ukatokea, na hapo ikamlazimu mwanamuziki huyo kuahirisha onesho lake, na kulisogeza wiki mbili mbele huku akiahidi asilimia 15 ya faida atakayopata, angeipeleka kwa familia ya Albert Mangwea.
Baada ya mazishi, Onesho la The Finest lilifanyika Juni 14, na baada ya hapo, MwanaFA hakuonekana akisema kwenye mitandao wala kwenye redio kuhusiana na mapato yake kwenye onesho hilo na kiasi gani alipeleka kwa Mama Mangwea. Tangu onesho hilo, huu ni mwezi wa tatu na ndipo gazeti moja la kila wiki likaandika kuhusiana na suala hilo, jambo ambalo linaendelea kuzungumzwa kila kukicha kwenye vyombo vya habari. Na ndipo gazeti hili liliamua kwanza kumtafuta Mwana FA na kuongea naye.
Kauli ya MwanaFA
Akiongea na Mwananchi, MwanaFA alikiri kuahidi kutoa fedha hizo na aliahidi asilimia 15 ya faida  itakayotokana na mapato ya onesho la The Finest.
“Nakiri kukosea jambo moja, nilipoahidi, niliongea na wanahabari lakini wakati wa kutoa, nilitoa bila kutangaza, na hii kutoa jamani ni moyo, haina haja kumtangaza mtu kwa kuwa umemsaidia au umempa pole”, alifafanua MwanaFA
Alisema katika mapato aliyoyapata kutokana na onesho hilo ambayo yalikuwa ni jumla ya shilingi 19.5 milioni, alitoa milioni tatu na kuzikabidhi kwa mama huyo, ingawa si taslimu, aliziingiza kwenye akaunti yake, katika benki ya Exim. Alifafanua kwamba alilifanya hili kwa moyo na hakuwa na nia ya  kujitangaza kwa hiyo alilimaliza akawa anaendelea na shughuli zake. Baada ya kauli hii, Mwananchi likapiga mguu mpaka Kihonda kwa mama yake Mangwea, Bi Denisia Costantine Mangwea
Mama Mangwea ashangaa!
Alipoulizwa kuhusiana na sakata hilo Mama Mangwea alikiri kwamba ameumia sana moyo baada ya kusikia ripoti ya kwamba MwanaFA anadaiwa hakutoa hizo pesa kwani alitoa kipindi kile kile cha msiba.
“Kabla hata ya arobaini, aliweka benki kisha akaja na mwenyewe, hakuna na waandishi kama wanavyofanya wenzake, alikuja mwenyewe tukaongea, na mara kwa mara tunawasiliana, wanataka kumtia doa kijana wa watu ni muungwana sana”, alifafanua mama Mangwea.


Kwa uthibitisho zaidi mama huyo alitoa risiti aliyokabidhiwa na MwanaFA ikionesha kiasi cha fedha alichotoa na tarehe halisi ambayo fedha hizo ziliwekwa kwenye akaunti yake.
“Naomba kwa niaba ya familia niwathibitishie alitoa na mngemwacha kijana wa watu aendelee na shughuli zake, kwani alitoa kwa nia njema na ndiyo maana hakutaka kuitangaza sana”, alimaliza mama huyo. Katika wiki mbili hizi vyombo mbali mbali, na hata kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na mjadala kuhusiana na ahadi hiyo ya MwanaFA iliyodaiwa kuwa hewa.
Source: Mwananchi

6 comments:

oakleyses said...

burberry outlet, nike outlet, oakley sunglasses, kate spade outlet, michael kors outlet online, tiffany and co, tiffany jewelry, michael kors outlet online, louis vuitton, christian louboutin, michael kors outlet, louis vuitton outlet, nike air max, ray ban sunglasses, louis vuitton, cheap oakley sunglasses, michael kors outlet online, gucci handbags, prada handbags, michael kors outlet, uggs on sale, longchamp outlet, tory burch outlet, ray ban sunglasses, christian louboutin shoes, uggs outlet, oakley sunglasses, christian louboutin uk, ray ban sunglasses, longchamp outlet, chanel handbags, nike free, ugg boots, uggs outlet, prada outlet, louis vuitton outlet, replica watches, oakley sunglasses wholesale, christian louboutin outlet, polo ralph lauren outlet online, jordan shoes, burberry handbags, nike air max, replica watches, ugg boots, oakley sunglasses, polo outlet, longchamp outlet

oakleyses said...

lululemon canada, ray ban pas cher, michael kors pas cher, burberry pas cher, sac vanessa bruno, north face, nike air force, hollister uk, coach outlet, abercrombie and fitch uk, nike air max uk, nike blazer pas cher, nike air max uk, new balance, coach outlet store online, nike roshe, true religion outlet, sac longchamp pas cher, timberland pas cher, true religion jeans, polo ralph lauren, mulberry uk, coach purses, true religion outlet, guess pas cher, nike tn, nike free run, sac hermes, michael kors, ray ban uk, hollister pas cher, north face uk, ralph lauren uk, nike air max, polo lacoste, converse pas cher, oakley pas cher, air max, replica handbags, true religion outlet, michael kors, kate spade, vans pas cher, michael kors outlet, louboutin pas cher, nike roshe run uk, hogan outlet, longchamp pas cher, jordan pas cher, nike free uk

oakleyses said...

longchamp uk, reebok outlet, celine handbags, iphone 6 plus cases, louboutin, ferragamo shoes, p90x workout, nike huaraches, hollister, giuseppe zanotti outlet, lululemon, jimmy choo outlet, babyliss, chi flat iron, north face outlet, bottega veneta, iphone 6s cases, nike roshe run, beats by dre, hermes belt, s6 case, nike air max, wedding dresses, iphone cases, oakley, asics running shoes, soccer shoes, ipad cases, ralph lauren, mont blanc pens, iphone 6 cases, nike trainers uk, ghd hair, abercrombie and fitch, nfl jerseys, mac cosmetics, vans outlet, herve leger, hollister clothing, mcm handbags, north face outlet, iphone 6s plus cases, valentino shoes, insanity workout, iphone 5s cases, instyler, timberland boots, new balance shoes, soccer jerseys, baseball bats

oakleyses said...

moncler, ugg uk, replica watches, moncler, louis vuitton, canada goose outlet, lancel, louis vuitton, karen millen uk, doudoune moncler, pandora charms, links of london, canada goose outlet, juicy couture outlet, moncler, vans, juicy couture outlet, ray ban, coach outlet, thomas sabo, converse, moncler outlet, marc jacobs, hollister, moncler uk, pandora jewelry, canada goose outlet, barbour uk, ugg pas cher, hollister, nike air max, canada goose jackets, swarovski, louis vuitton, ugg, pandora jewelry, converse outlet, swarovski crystal, wedding dresses, canada goose, canada goose, louis vuitton, moncler, ugg,uggs,uggs canada, barbour, canada goose, louis vuitton, toms shoes, moncler outlet, ugg,ugg australia,ugg italia, gucci, pandora uk, supra shoes

oakleyses said...

nike air max, longchamp outlet, louis vuitton, nike outlet, prada handbags, ray ban sunglasses, jordan shoes, ugg boots, tiffany and co, ray ban sunglasses, polo outlet, nike free, christian louboutin outlet, louis vuitton, prada outlet, chanel handbags, ray ban sunglasses, christian louboutin uk, nike air max, longchamp outlet, louis vuitton outlet, tiffany jewelry, kate spade outlet, uggs on sale, oakley sunglasses, louis vuitton outlet, christian louboutin shoes, longchamp outlet, polo ralph lauren outlet online, gucci handbags, replica watches, replica watches, tory burch outlet, oakley sunglasses wholesale, ugg boots, oakley sunglasses, cheap oakley sunglasses, oakley sunglasses, christian louboutin, louis vuitton outlet

oakleyses said...

michael kors outlet online, michael kors outlet online, uggs outlet, uggs outlet, michael kors outlet online, michael kors outlet, michael kors outlet, burberry handbags, michael kors outlet online, burberry outlet