Sunday, October 13, 2013

Mwakyembe ajitosa kuokoa mabilioni kutokana na mgomo wa malori


Serikali imesema mgomo wa madereva wa malori umeyumbisha uchumi wa nchi na kuiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kufanyakazi saa 24, Bandarini Dar es Salaam ili kupunguza athari zilizilojitokeza.

Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) na Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), mapema wiki hii kilisimamisha kusafirisha mizigo na abiria nchi nzima kutokana na Wizara ya Ujenzi kuondoa nafuu ya kutolipa tozo ya uzito wa magari uliozidi asilimia tano ya uzito unaokubaliwa kisheria. 

Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrisson Mwakyembe, alitoa agizo hilo wakati akipokea meli kubwa kutoka kampuni ya Maersk ya nchini Denmark yenye uwezo wa kubeba kontena 4,500 ambayo ni mara ya kwanza kuingia nchini kwa ajili ya majaribio.


Mwakyembe ingawa hakutaja hasara iliyopatikana, alisema ingawa malori hayo yameanza kufanyakazi, lakini athari iliyojitokeza ni kubwa kiuchumi na kukiagiza kitengo cha mizigo cha TRA kufanyakazi saa 24 kuokoa hali ya uchumi.

"Watakaotuangusha kidogo ni TRA, nikitoka hapa nitaenda kuzungumza nao ili ikiwezekana wenye mabenki walete mobile bank zao kutoa huduma hata kama ni saa nane ya usiku," alisema Dk. Mwakyembe na kuongeza "tena wafanye saa 24 hata katika kipindi cha sikukuu maana wamezoe siku za weekend (mwisho wa wiki) wanafanyakazi hadi saa sita.”

Alisema lengo ni kuhakikisha mizigo iliyobaki inamalizika kwa wakati pamoja na kuziba athari zilizojitokeza katika kipindi chote cha mgomo.

Alisema kipindi cha mgomo kulijitokeza usumbufu mkubwa kwa wasafirishaji hasa katika Bandari ya Dar es Salaam.

“Leo tumefungua ukurasa mpya baada ya taifa kugubikwa na mgomo mkubwa wa madereva wa malori, tunashukuru Mungu tatizo hili tumelimaliza, ninachoomba sasa ni kushirikiana kwa pamoja kuchapa kazi, ili kuziba kasoro zote zilizojitokeza katika kipindi chote cha mgomo,” alisema.

Alisema katika siku za mgomo uliodumu kwa siku nne, Bandari ya Dar es Salaam ilisongamana na mizigo, lakini mpaka sasa hali ni shwari na mizigo inaendelea kuondolewa kama ilivyokuwa hapo awali.

Aidha, alisema usiku wa kuamkia juzi, juhudi za ziada zilifanyika kuondoa mizigo iliyokuwa imesongamana bandarini hapo na kuwasifia wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) kufanyakazi usiku kucha kutatua tatizo la mrundikano wa mizigo bandarini.

TATOA, TABOA WAOMBA RADHI WANANCHI
Katika tamko lao jana ambalo NIPASHEilifanikiwa kuliona, TATOA ilidai kuwa wadau ambao awali walishirikiana kuweka unafuu wa tozo hili hawakushirikishwa kuliondoa, na pia tamko la wizara linakinzana na sheria ya mwaka 2001.

"Sisi kama TATOA tunaamini kuwa sekta binafsi na serikali zinapaswa kushirikiana katika kufanya maamuzi, hasa ya kisera, ambayo yanaathiri sekta kwa namna yoyote ile," lilisema tamko hilo.

Vyama hivyo vimeomba radhi kwa wananchi, wateja na wadau wote kwa usumbufu walioupata kwa siku nne zilizopita na kusema kuwa sio lengo la TATOA au TABOA, kushindana na serikali au kutotii sheria. Na kwamba wako tayari kutoa ushirikiano utakaotakiwa na serikali katika kumaliza jambo hili na meza ya majadiliano ndio suluhisho zuri. 

MELI KUBWA YAINGIA NCHINI
Kuhusu meli iliyoingia jana, Dk. Mwakyembe alisema ina ukubwa wa mita 250, sawa na viwanja viwili na nusu vya mpira ambayo itakuwa inaingiza mizigo nchini.

Dk. Mwakyembe alisema ujio wa meli hiyo ni ujumbe kuwa biashara inachanganya kwa wateja wengine waliokuwa hawapitishii bidhaa zao Tanzania na kuishia nchi za jirani.

Alisema meli hiyo itatoa fursa kwa wateja kupitishia biashara zao katika bandari ya Dar es Salaam na kwamba hiyo ni dalili nzuri inayoonyesha Tanzania inakua kiuchumi.

“Tanzania tulikuwa tumezoea kwamba sisi ni wa kutumia meli ndogo ndogo tu, lakini ni jambo jema kwamba tumethubutu kwa mara kwanza, tumeweka historia kwa kupokea meli kubwa kama hii,” alisema Dk Mwakyembe.
Aliongeza: “ Huu ni mwanzo tu, tutaendelea kujionea mambo mazuri zaidi ya haya, kinachotakiwa ni kujipanga na kuchapa kazi.”

Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania(TPA), Madeni Kipande, alisema ujio wa meli hiyo utapunguza gharama za uendeshaji tofauti na ilivyo kwa meli ndogo ndogo ambazo wamekuwa wakitumia.
Alisema kutumia meli ndogo kunasababisha gharama kubwa zaidi na kwamba ni wakati umefika kwa makampuni mengine kutafuta meli kama hizo.

Pia alisema ni changamoto kwa serikali kuhakikisha inatafuta vifaa vya kisasa vya kupakulia mizigo vitakavyoendana na hadhi ya meli.

Meneja uendeshaji wa Kampuni hiyo ya Maersk, Amosi Mwasumbwe, alisema mafanikio ya ujio wa meli hiyo hapa Tanzania, yametokana na ushirikiano kati ya Tanzania kampuni hiyo.

Alisema meli hiyo itaisaidia Tanzania kuokoa baadhi ya gharama wakati ikitumia meli ndogo na kwamba kama itafanya jitihada za kuongeza nyingine za aina hiyo, uchumi wake utaongezeka kwa kasi zaidi.

Kwa upande wake Nahodha wa meli hiyo, Abdul Mwingamno ambaye ni Mtanzania alisema kuwa meli hiyo ametokea Angola na iliwasili jana majira ya saa 3 asubuhi ikiwa na makontena 4,500

6 comments:

oakleyses said...

burberry outlet, nike outlet, oakley sunglasses, kate spade outlet, michael kors outlet online, tiffany and co, tiffany jewelry, michael kors outlet online, louis vuitton, christian louboutin, michael kors outlet, louis vuitton outlet, nike air max, ray ban sunglasses, louis vuitton, cheap oakley sunglasses, michael kors outlet online, gucci handbags, prada handbags, michael kors outlet, uggs on sale, longchamp outlet, tory burch outlet, ray ban sunglasses, christian louboutin shoes, uggs outlet, oakley sunglasses, christian louboutin uk, ray ban sunglasses, longchamp outlet, chanel handbags, nike free, ugg boots, uggs outlet, prada outlet, louis vuitton outlet, replica watches, oakley sunglasses wholesale, christian louboutin outlet, polo ralph lauren outlet online, jordan shoes, burberry handbags, nike air max, replica watches, ugg boots, oakley sunglasses, polo outlet, longchamp outlet

oakleyses said...

lululemon canada, ray ban pas cher, michael kors pas cher, burberry pas cher, sac vanessa bruno, north face, nike air force, hollister uk, coach outlet, abercrombie and fitch uk, nike air max uk, nike blazer pas cher, nike air max uk, new balance, coach outlet store online, nike roshe, true religion outlet, sac longchamp pas cher, timberland pas cher, true religion jeans, polo ralph lauren, mulberry uk, coach purses, true religion outlet, guess pas cher, nike tn, nike free run, sac hermes, michael kors, ray ban uk, hollister pas cher, north face uk, ralph lauren uk, nike air max, polo lacoste, converse pas cher, oakley pas cher, air max, replica handbags, true religion outlet, michael kors, kate spade, vans pas cher, michael kors outlet, louboutin pas cher, nike roshe run uk, hogan outlet, longchamp pas cher, jordan pas cher, nike free uk

oakleyses said...

longchamp uk, reebok outlet, celine handbags, iphone 6 plus cases, louboutin, ferragamo shoes, p90x workout, nike huaraches, hollister, giuseppe zanotti outlet, lululemon, jimmy choo outlet, babyliss, chi flat iron, north face outlet, bottega veneta, iphone 6s cases, nike roshe run, beats by dre, hermes belt, s6 case, nike air max, wedding dresses, iphone cases, oakley, asics running shoes, soccer shoes, ipad cases, ralph lauren, mont blanc pens, iphone 6 cases, nike trainers uk, ghd hair, abercrombie and fitch, nfl jerseys, mac cosmetics, vans outlet, herve leger, hollister clothing, mcm handbags, north face outlet, iphone 6s plus cases, valentino shoes, insanity workout, iphone 5s cases, instyler, timberland boots, new balance shoes, soccer jerseys, baseball bats

oakleyses said...

moncler, ugg uk, replica watches, moncler, louis vuitton, canada goose outlet, lancel, louis vuitton, karen millen uk, doudoune moncler, pandora charms, links of london, canada goose outlet, juicy couture outlet, moncler, vans, juicy couture outlet, ray ban, coach outlet, thomas sabo, converse, moncler outlet, marc jacobs, hollister, moncler uk, pandora jewelry, canada goose outlet, barbour uk, ugg pas cher, hollister, nike air max, canada goose jackets, swarovski, louis vuitton, ugg, pandora jewelry, converse outlet, swarovski crystal, wedding dresses, canada goose, canada goose, louis vuitton, moncler, ugg,uggs,uggs canada, barbour, canada goose, louis vuitton, toms shoes, moncler outlet, ugg,ugg australia,ugg italia, gucci, pandora uk, supra shoes

oakleyses said...

nike air max, longchamp outlet, louis vuitton, nike outlet, prada handbags, ray ban sunglasses, jordan shoes, ugg boots, tiffany and co, ray ban sunglasses, polo outlet, nike free, christian louboutin outlet, louis vuitton, prada outlet, chanel handbags, ray ban sunglasses, christian louboutin uk, nike air max, longchamp outlet, louis vuitton outlet, tiffany jewelry, kate spade outlet, uggs on sale, oakley sunglasses, louis vuitton outlet, christian louboutin shoes, longchamp outlet, polo ralph lauren outlet online, gucci handbags, replica watches, replica watches, tory burch outlet, oakley sunglasses wholesale, ugg boots, oakley sunglasses, cheap oakley sunglasses, oakley sunglasses, christian louboutin, louis vuitton outlet

oakleyses said...

michael kors outlet online, michael kors outlet online, uggs outlet, uggs outlet, michael kors outlet online, michael kors outlet, michael kors outlet, burberry handbags, michael kors outlet online, burberry outlet