Sunday, September 11, 2011

Ni maafa ya kiistoria Zanzibar

Watu 187 wafia baharini Zanzibar baada ya meli kuzama


Waokoaji huko Zanzibar wakibeba miili ya watu waliofariki tayari kuipeleka kutambuliwa na wapendwa wao
 Watu wapatao 187 hadi sasa wamethibitika kufariki dunia baada ya meli Mv Spice kuzama alfajiri ya  kuamkia jana huko Zanzibar . Meli hiyo ilizama baharini baada ingini zake kuzimika ikiwa katikati ya bahari.

Taarifa zinasema watu wapatao 620 wameokolewa kwenye Meli hiyo iliyokuwa inatoka kisiwa cha  Unguja kwenda kisiwa kingine cha Pemba vyote vya Zanzibar.

Tayari serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetangaza maombolezo ya siku tatu kwa ajili msiba huo mzito ulioikumba Tanzania.

Rais wa Zanzibar Dk. Ally Mohamed Shein amesema bendera zote zitapepea nusu mlingoti wakati wa maombolezo hayo.

Naye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ametutumia salamu za rambi rambi kwa wananchi wa Zanzibar kufuatia msiba huo mzito na kutangaza pia maombelezo ya siku tangu ambapo pia bendera zote katika Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zitapepea nusu mlingoti
Hadi sasa juhudi za uokoji zinaendelea kutafuta kama kuna watu zaidi walio hai na kutafuta miili iliyozama baharini.Watu wengi waliookolewa ni wale waliokuwa wakielea wakitumia magodoro na vitu vingine vinavyoolea kama majokofu na vingine.

Baadhi ya watu waliokuwa kwenye meli ya Mv Spice wakielea kwa kutumia godoro katikati ya bahari wakisubiri kuokolewa
Baadhi ya watu waliookolewa katika ajali hiyo wakiwa wamejifunika mablanketi

Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wenye ndugu zao waliosafiri wakisubiri taarifa za ndugu zao waliopata ajali hiyo ya meli

Vikosi wa jeshi vikisaidia uokoaji na kubeba miili ya walifariki dunia katika ajili hiyo ya meli