Waombolezaji wakiubeba mwili wa Marehemu Siraji Kaboyonga |
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya
leo ameungana na mamia ya waombolezaji kumzika
aliyepata kuwa Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), Hayati Siraji Juma Kaboyonga.
Marehemu
Kaboyonga ambaye amezikwa kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam, alifariki
dunia usiku wa Jumanne ya wiki hii kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
kwa ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka 63.
Miongoni
mwa waombolezaji walioshiriki mazishi ya leo ya Marehemu Kaboyonga, ambaye
mpaka kifo chake alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mifuko
ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), alikuwa Rais wa Awamu ya Pili ya Uongozi wa
Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi.
Marehemu
Kaboyonga alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya Chama cha
Mapinduzi kati ya 2005 na 2010 na katika salamu zake za rambirambi jana, Rais
Kikwete alimwelezea marehemu kama mtumishi wa umma wa mfano wa kuigwa ambaye
uwezo wake wa uongozi ulijionyesha dhahiri wakati wa kipindi chake cha ubunge
na kwenye nafasi nyingine za umma alizopata kuzishikilia katika maisha yake.
No comments:
Post a Comment