THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR
ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
Kikwete atoa maelekezo kuhusu kodi ya simu za mkononi
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameagiza Wizara za
Serikali zinahusika na kodi na mawasiliano pamoja na makampuni ya simu za
mikononi nchini kukutana mara moja kutafuta jinsi gani ya kumaliza mvutano wa
kodi mpya ya kadi za simu hizo za mikononi.
Rais kikwete ametoa
maelekezo hayo jioni ya leo, Jumanne, Julai 23, 2013 wakati alipokutana na
viongozi wa Wizara ya Fedha, Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na
wawakilishi wa makampuni ya simu ya TTCL, Airtel, Vodacom, Tigo na Zantel
katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amesema
kuwa lengo kuu la mkutano huo wa pamoja kati ya Wizara hizo za Serikali na
makampuni ya simu yawe ya kupendekeza jinsi gani ya kuziba pengo la Sh. Bilioni
178 ambazo zitapotea katika Bajeti iwapo kodi hiyo kwa kadi za kuongelea za
simu za mikononi italazimika kufutwa na Serikali kupitia marekebisho kwenye
Muswada wa Fedha wa Bajeti ya Mwaka 2013/2014.
Rais Kikwete
amewaambia wawakilishi wa pande hizo mbili kuwa huwezi tena kuifuta moja kwa
moja kodi hiyo bila kutafuta njia nyingine za kupata fedha za kujaza pengo hilo
la Sh. Bilioni 178 ambazo tayari Bunge limezipangia matumizi.
“Nawaombeni kaeni
pamoja, wekeni bongo zenu pamoja, wekeni akili yenu pamoja tutafute namna gani
tunaweza kujaza pengo hili la Sh. Bilioni 178 endapo tutakubaliana kuwa kodi
hii inawabebesha wananchi mzigo mzito na kuwa pengine menejimenti ya kodi
yenyewe ni ngumu,” Rais Kikwete
amewaambia wawakilisho hao.
Katika Bajeti ya
Serikali ya mwaka 2013/2014, Serikali imeweka kodi ya Sh. 1,000/= kwa mwezi kwa
kila mtumiaji simu kwa ajili ya kufanya mawasiliano kwa kutumia simu ya
mkononi.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
23 Julai, 2013
No comments:
Post a Comment