Wednesday, November 24, 2010

Mambo hadharani Kikwete awapa ulaji Sitta, Tibaijuka na Nahodha, atangaza Baraza la Mawaziri


Shamsi Vuai Nahodha


Hatimaye Rais Jakaya Kikwete ametangaza baraza la mawaziri ambapo sura mpya na nyingine za zamani zimeonekana.

Katika Baraza hilo amemteua Spika aliyepita Samweli Sitta kuwa waziri wa Afrika Mashariki huku Shamsi Vuai Nahodha akipewa Wizara ya Mambo ya ndani.
Wengine ni Profesa Anne Tibaijuka aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi huku John Magufuli akiteuliwa kuongoza wizara mpya ya ujenzi itakayohusika na barabara pamoja na viwanja vya ndege.

Baraza kamili ni kama ilivyo hapa chini.
Ofisi ya Rais Utawala Bora ni Mathias Chikawe, Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Stephen Wassira


Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Hawa Ghasia

Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Samia Suluhu, Mazingira Dr. Terezya Luoga Hovisa


Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi,Uwekezaji na Uwezeshaji Dr. Mary Nagu

Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)George Huruma Mkuchika,Naibu ni Aggrey Mwanri na Kassim Majaliwa.


Wizara ya Fedha Mustapha Mkulo Naibu ni Gregory Teu na Pereira Ame Silima

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ni Shamsi Vuai Nahodha Naibu ni Balozi Khamis Suedi Kagasheki

Wizara ya Katiba na Sheria Celina Kombani

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe, Naibu ni Mahadhi Juma Mahadhi

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr. Hussein Ali Hassan Mwinyi

Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. Mathayo David Mathayo na Naibu ni Benedict Ole Nangoro

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ni Prof. Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu ni Charles Kitwanga.

Anne Tibaijuka
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ni Prof. Anna Tibaijuka na Naibu ni Goodluck Ole Madeye

Wizara ya Maliasili na Utalii ni Ezekiel Maige

Wizara ya Nishati na Madini ni William Mganga Ngeleja na Naibu ni Adam Kigoma Malima

Wizara ya Ujenzi ni Dr. John Pombe Magufuli na Naibu ni Dr. Harrison Mwakyembe


Wizara ya Uchukuzi Omari Nundu na Naibu ni Athumani Mfutakamba

Wizara ya Viwanda na Biashara ni Dr. Cyril Chami na Naibu ni Lazaro Nyalandu

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni Dr. Shukuru Kawambwa na Naibu ni Philipo Mulugo

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ni Dr. Haji Hussein Mpanda na Dr. Lucy Nkya

Wizara ya Kazi na Ajira ni Gaudensia Kabaka na Naibu Makongoro Mahanga

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ni Sophia Simba na Naibu ni Umi Ali Mwalimu

Wizara ya Habari, Vijana na Michezo ni Emmanuel John Nchimbi na Naibu ni Dr. Fenella Mukangara

Mhe.Samwel Sitta
Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni Samuel John Sitta na Naibu ni Dr. Abdallah Juma Abdallah

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ni Prof. Jumanne Maghembe na Naibu ni Christopher Chiza

Wizara ya Maji ni Prof. Mark James Mwandosya na Naibu ni Eng. Gerson Lwinge

No comments: