Monday, December 13, 2010

Dk. Remmy Ongala afariki duniaKuna taarifa za kusikitisha kuwa mwanamuzi maarufu nchini Tanzania Ramadhan Ongala maarufu Dk. Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.

Dk. Remmy atakumbukwa kwa kama mwanamuzi mkongwe ambaye ameimba nyimbo nyingi zenye ujumbe wa kugusa maisha ya kawaida ya jamii kama vile 'siku ya kifo" , 'narudi nyumbani' na nyingine nyingi.

Kabla ya mauti kumkuta Marehemu Dk. Remmy alikuwa ni muumini wa makanisa ya kilokole baada ya kuamua kuokoka ambapo pia alianza kuimba nyimbo za injili za kumtukuza Mungu.

Bwana Ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe Amen.