Saturday, December 4, 2010

Gbagbo kuapishwa pamoja na kushindwa uchaguzi Ivory Cost

Alassane Ouattara


Kuna taarifa kuwa Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Cost anatarajiwa kuapishwa leo pamoja na kushindwa kwenye uchaguzi Mkuu ulifanyika hivi karibuni.

Katika uchaguzi wa marudio mpinzani wake Alassane Ouattara (pichani) ndiye anayeaminika kushinda lakini Baraza la Katiba la nchi hiyo likakataa kumtangaza na kutangaza kuwa Gbagbo ndiye alisheshinda.

Inaaminika Ouattara alishinda kwa asilimia 54.1 dhidi ya 45.1 alizopata Rais Gbagbo.

Wafuasi wa Rais Gbagbo walijaribu kuzuia kutoka kwa matokeo hayo yaliyocheleweshwa, wakidai umefanyika wizi wa kura katika eneo la kaskazini.

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limetaka pande zote kuonesha uvumilivu.

Tangazo la matokeo ya uchaguzi uliofanyika Jumapili, limecheleweshwa sana, na hivyo kusababisha kuwepo kwa hali ya wasiwasi nchini humo.

Wafuasi wa Gbagbo walijaribu kuzuia matokeo hayo kutoka, wakisema umefanyika wizi katika eneo la kaskazini ambapo Bw Ouattara ana umaarufu mkubwa.

Upande wa kaskazini unadhibitiwa na waasi wa zamani.

No comments: