Friday, December 3, 2010

Harambee yasambaratishwa na Ethiopia 2- 1Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imesambaratishwa na timu ya taifa ya Ethiopia kwa kufungwa magoli 2-1 katika michi ya kukata na shoka ya kombe la Cecafa senior kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Harambee Star sasa imepoteza matumaini ya kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya mashindano hayo na hivyo kusubiri kama inaweza kuwa miongoni mwa timu mbili za mwisho zilizofanya vizuri best loosers kama itashinda mechi ya Jumapili dhidi ya timu ya taifa ya Uganda The Cranes.

No comments: