Sunday, December 5, 2010

Mbeki yupo Ivory Cost kusuluhisha mgogoro


Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini Thabo Mbeki yupo nchini Ivory Cost kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro unaofukuta nchini humo baada ya Rais Laurent Gbagbo kuapishwa hapo jana japo alishindwa katika uchaguzi wa marudio uliofanyika hivi karibuni.

Rais Mbeki aliwahi kusuluhisha mgogoro nchini humo wakati alipokuwa rais lakini wapinzani wa Ivory Cost hata kwa wakati huo walimwona alikuwa anaegemea upande wa Rais Gbagbo.

Hivi sasa Ivory Cost ipo katika hali ya sitofahamu baada ya mvutano baina ya Rais Gbagbo na Alassane Ouattara aliyetangazwa na tume ya uchuguzi nchini humo kuwa ndiye mshindi lakini baadae mahakama ya katiba ikabatilisha ushindi huo.

Tayari mahasimu hao kila mmoja kwa upande wake amekwishatangaza kuwa ndiye rais na kila mmoja amekwishateua Waziri Mkuu.

No comments: