Sunday, January 9, 2011

Sudan ya kusini wapiga kura


Wapiga kura Kusini mwa Sudan wamejitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni itakayosababisha Sudan Kusini kuwa nchi huru na jipya kabisa kote duniani.

Maelfu ya wapiga kura walipiga foleni katika vituo vya kupiga kura hata kabla ya vituo hivyo kufunguliwa.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir (pichani mwenye kofia), alikuwa miongoni wa waliotangulia mapema kupiga kura.

Raia wa Kusini wanaoishi kaskazini mwa Sudan nao pia watapiga kura lakini hakuna shamrashamra za kisiasa kama ilivyo Sudan ya Kusini.

Wengi wameyahama makazi yao kaskazini kurejea eneo la mababu zao ambayo ni Sudan Kusini.

Lakini baadhi ya raia wa kusini mwa Sudan wameelezea wasiwasi kuhusu mustakabali wao ikiwa Sudan ya kusini itajitenga. (BBC Swahili)

No comments: